Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. KANGI A. LUGOLA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Mradi mkubwa wa Maji katika Jimbo la Mwibara utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. KANGI A. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, kwanza, niishukuru Serikali ya Mama, Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kuona umuhimu wa kuwapa maji Wanamwibara wapatao 200,000. Sasa kwa kuwa usanifu ulishakamilika zaidi ya miaka mitatu sasa, na kwa sababu usanifu ni chanzo cha kujenga matumaini kwa wananchi kupata maji, kwa nini, sasa Serikali baada ya kuona utafutaji wa fedha kwa wafadhili unachukua muda mrefu, kwa nini, wasitenge bajeti kwenye fedha za Serikali ili waanze kujenga mradi huo awamu kwa awamu ili matumaini yaliyojaa kwa Wanamwibara yasije yakapotea?

Mheshimiwa Spika, la pili, kwa kuwa mradi huu umechelewa na wananchi wa Mji wa Kibara ambapo ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Vijijini ni mradi ambao una changamoto nyingi mabomba kupasuka, wakati mwingine mitambo haiwaki.

Mheshimiwa Spika, je, uko Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari baada ya Bunge hili Tukufu litakapoahirishwa kuja Mwibara na ikiwezekana kwenda nami mguu kwa mguu ili akajionee changamoto za mradi huu ili wananchi wapate maji? Ahsante. (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nianze na swali la pili. Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, daima imekuwa ikihakikisha kwamba inafika maeneo ya changamoto ili kujionea ukubwa wa namna ambavyo wananchi wanahangaika.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, niko tayari kwenda na Mheshimiwa Kangi Lugola, mguu kwa mguu kwenye Jimbo lake la Mwibara kuhakikisha kwamba tunatoa kauli ya Serikali baada ya kujiridhisha na changamoto za tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza ni ushauri ambapo Mheshimiwa Mbunge ameshauri tuweke katika bajeti ya Serikali. Ni kweli kabisa kwa sasa sekta ya maji tunakuja na kitu kinaitwa alternative financing, maana yake hatuwezi kutegemea fedha za wadau pekee yake, lakini pia hatuwezi kutegemea fedha za Serikali pekee yake. Tunatoa fursa kwa wadau wengine ambao wanaweza kuingia kwenye sekta ya maji tukashirikiana kwa mfumo wa PPP. Kwa hiyo, tunaamini kwamba kuna njia nyingi ambazo tunakwenda kutekeleza miradi hii.

Mheshimiwa Spika, kikubwa ni kwamba mradi huu lazima uzingatie maslahi na uzingatie sera yetu ya Maji ya 2002 toleo la mwaka 2025 kwenye security ya maji ambao hatuwezi kwenda kichwa kichwa ku-engage private sector bila kuwa na tahadhari, lakini tutaendelea kuangalia namna gani tutafanya. Ahsante sana.