Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 2 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 34 | 2026-01-28 |
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. KANGI A. LUGOLA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Mradi mkubwa wa Maji katika Jimbo la Mwibara utaanza?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda vijiji 30 vya Jimbo la Mwibara Wilayani Bunda. Miongoni mwa kazi zinazotarajiwa kutekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake) na mtambo wa kutibu maji (treatment plant) mwenye kuzalisha lita milioni 35.7, ujenzi wa nyumba ya mitambo (booster station), ujenzi wa matanki 10 yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 19.3, ulazaji wa mtandao wa bomba zaidi ya umbali wa kilometa 500, ujenzi wa mbauti 30 za kunyweshea mifugo, ujenzi wa vituo 124 vya kuchotea maji sanjari na maunganisho kwa wateja 5,000 wa majumbani.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza utekelezaji wa mradi huo unaotarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 94 ambapo utanufaisha zaidi ya wananchi 200,000 wa Jimbo la Mwibara.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved