Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Maji wa Mwanga B – Kasulu?

Supplementary Question 1

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri. Pia, ninaomba nitumie nafasi hii kuishukuru kwa dhati Wizara ya Maji kwa namna ambavyo inafuatilia miradi katika jimbo langu kwa sababu kule hali bado ni tete.

Mheshimiwa Spika, swali langu la nyongeza. Kwa kuwa mabomba hayo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameyazungumza yenye urefu wa kilometa 52 yalipokelewa tangu mwezi Mei, 2025, je, ni lini hasa Serikali itaendelea na utekelezaji wa awamu zinazofuata ili wananchi hawa wa Mwanga, Nyachidima, Kabanga, Nyalumanga, Kimombwa pamoja na Kidiama waweze kunufaika kwa sababu wanapata adha kubwa ya maji? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Prof. Joyce Lazaro Ndalichako, Mbunge wa Kasulu Mjini, kwa kazi kubwa ambayo anatupatia ushirikiano mzuri sana tunapofanya ziara katika jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, nitumie Bunge lako Tukufu kuwahakikishia wananchi kutoka mitaa hii sita: Mwanga B, Mganza, Msambala, Nyachidima, Kimombwa na Kigondo, kuwa mradi huu wenye gharama ya shilingi bilioni 2.9, tayari mabomba yameshafikishwa eneo la utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, Serikali imejipanga kupeleka fedha kwa ajili ya kwenda kumalizia mradi huu ili wananchi wa mitaa hii waweze kupata huduma ya majisafi na salama sambamba na kuongeza upatikanaji wa maji ambao kwa sasa kwa Kasulu Mjini ni 71%, na sambamba na mradi wa miji 28 ambao unaendelea pale Kasulu utafikisha huduma ya maji kufikia 95%.