Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 2 Water and Irrigation Wizara ya Maji 33 2026-01-28

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Maji wa Mwanga B – Kasulu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa maji Mwanga B uliopo Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambapo hadi sasa Mkandarasi ameshapeleka mabomba yote ya mradi yenye urefu wa jumla ya kilometa 52 eneo la mradi. Kazi nyingine zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na kubadili mfumo wa nishati ya umeme wa jua kwenda umeme wa gridi kwa ajili ya uzalishaji maji sambamba na ujenzi wa chemba za ukaguzi wa mitambo ya mabomba.

Mheshimiwa Spika, Serikali inahakikisha inapeleka fedha za utekelezaji wa mradi huo ili uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi waishio katika mitaa sita ya Mwanga B, Mganza, Msambala, Nyachidima, Kimombwa na Kigondo, ahsante.