Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Maji ya mserereko katika Kijiji cha Kapalala Kata ya Kapalala - Nsimbo?
Supplementary Question 1
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa visima viwili havifanyi kazi kabisa, kisima kimoja kinatoa maji ya kusuasua na wananchi wa Kapalala wana adha kubwa ya maji, ni nini mikakati ya Serikali kuhakikisha vile visima viwili vinatoa maji kwa dharura ili wananchi wa Kapalala waweze kupata maji? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Kwa kuwa maji ya mserereko mpaka sasa hivi kwenye bajeti mpango haupo, je, katika bajeti ijayo ya Serikali mpango huo utawekwa ili wananchi wa vijiji vyote saba waweze kupata manufaa ya majisafi na salama? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda nimpongeza sana Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo kwa kazi kubwa anayoifanya kuwatetea wananchi wake wa Jimbo lake la Nsimbo.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa, kwanza upatikanaji wa huduma ya maji katika Jimbo la Nsimbo kwa sasa ni 74% na ninafahamu mradi huu utakapokamilika utaweza kusaidia kutoka vijiji 23 vinavyopata huduma ya maji, lakini katika vijiji tisa ambavyo vitahudumiwa na huu mradi, vijiji vitano vina huduma ambayo inasuasua, na ni vijiji vinne ndivyo ambavyo hawana huduma ya maji kabisa.
Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kuwa huu mradi tunaenda kuhakikisha kwamba unakamilika. Pia huu mradi wa mserereko tunaenda kuuingiza kwenye bajeti ya fedha ya 2026/2027 ili kuhakikisha wananchi wake wanaendelea kupata huduma ya majisafi na salama, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved