Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 2 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 32 | 2026-01-28 |
Name
Anna Richard Lupembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Primary Question
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka Maji ya mserereko katika Kijiji cha Kapalala Kata ya Kapalala - Nsimbo?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya upungufu wa maji kwa wananchi wa Kijiji cha Kapalala Kata ya Kapalala kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani Mpanda. Kijiji hicho kwa sasa kinapata huduma ya maji kupitia visima vitatu vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita 23,742 kwa siku wakati mahitaji ya wananchi wa kijiji hicho ni lita 72,675 kwa siku.
Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa mradi wa kutumia chanzo cha maji ya mserereko cha Ikolongo ambapo unatarajia kunufaisha vijiji tisa Wilayani Mpanda kikiwemo Kijiji cha Kapalala. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huo unaotarajia kugharimu takribani shilingi bilioni saba.
Mheshimiwa Spika, ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved