Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kakulu Burchard Kakulu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. KAKULU B. KAKULU aliuliza: - Je, lini upanuzi wa Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala Rangi Tatu – Kongowe unatarajiwa kukamilika?

Supplementary Question 1

MHE. KAKULU B. KAKULU: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwanza kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini pia nichukue nafasi hii kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Mbagala kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza kwa kutusaidia kujenga ile barabara. Kwa kweli ilikuwa ni changamoto kubwa, ilisababisha msongamano mkubwa na ajali nyingi katika Kilima kile cha Mto Kizinga. Kwa hiyo, tunaishukuru sana Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu hayo mazuri, swali moja tu la nyongeza. Ninafahamu na wote tunajua umuhimu wa barabara inayounganisha pale Kongowe kutoka Kongowe kuelekea Kivukoni katika Jimbo la jirani la Kigamboni, na umuhimu wake hasa katika kulisha viwanda vilivyopo Kigamboni katika eneo la Kisarawe II na viwanda vilivyopo katika eneo la Mwandege pamoja na eneo la Mkuranga.

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali inaona umuhimu pia wa kupanua hii barabara kutoka Kongowe kwenda Kigamboni ili kusaidia kuhudumia hivi viwanda na shughuli nyingine za wananchi? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, kwanza nipokee pongezi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, kwa kutambua kazi kubwa ambayo anaifanya na hasa kuondoa changamoto ya msongamano wa barabara kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na kulijenga hilo daraja la Mzinga ambalo muda siyo mrefu tunaanza kulijenga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, hii barabara ya Kongowe kwenda Kivukoni ipo kwenye mpango wa kuondoa misongamano (decongestion) ya miji ikiwepo Mji wa Dar es Salaam ikiwepo pamoja na hiyo barabara ya Kongowe – Kivukoni.

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAKULU B. KAKULU aliuliza: - Je, lini upanuzi wa Barabara ya Kilwa kuanzia Mbagala Rangi Tatu – Kongowe unatarajiwa kukamilika?

Supplementary Question 2

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali inaenda kupanua barabara ya Tanga – Segera - Chalinze na hasa ukizingatia sasa hivi kumekuwa na msongamano mkubwa wa malori kwenye barabara hiyo? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli barabara ya Kaskazini ambayo ni T-2, kuanzia Chalinze kwenda Segera – Tanga, lakini hata kwenda Korogwe ni barabara ambazo zilijengwa zamani na ni finyu.

Mheshimiwa Spika, kinachofanyika sasa hivi ni kuifanyia usanifu ili iweze kufanyiwa matengenezo ama ukarabati mkubwa ikiwa ni pamoja na kuipanua na tunatambua kwa kweli kulingana na kazi zinazofanyika sasa hivi na Awamu ya Sita, magari yameongezeka na magari makubwa sana yanapita kwenye hizo barabara. Kwa hiyo, tuna kila wajibu wa kufanyia marekebisho barabara zetu ikiwepo na hiyo barabara ya Segera - Tanga.