Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: - Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umefikia katika hatua gani?

Supplementary Question 1

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri, ninaomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kibaha – Mlandizi – Chalinze imekuwa na foleni kubwa sana isiyomithilika, tena ni ya mara kwa mara. Je, ni upi mkakati wa muda mfupi wa Serikali kuhakikisha tunamaliza kadhia hiyo ya foleni?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Fursa ya mageuzi makubwa ya Bandari yetu ya Dar es Salaam imesababisha usafirishaji wa mizigo mingi kupitia Barabara hii ya Morogoro na kusababisha foleni kubwa sana. Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa Chalinze – Morogoro Express Way?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana aliyoyatoa kwa Waheshimiwa Wabunge kwenye swali la kwanza na katika swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani linalohusu Kibaha – Chalinze.

Mheshimiwa Spika, kwanza kuhusu mkakati wetu wa muda mfupi, tumekubaliana katika Wizara ya Ujenzi kwamba, tunayo barabara ya zamani ambayo mara baada ya kutengeneza barabara mpya tuliiacha. Tumepata fedha Serikalini tunaitengeneza kuwa ni barabara mbadala ili kusudi barabara kuu inapofunga, watu wawe na uwezo wa kupita katika barabara ile ya zamani inayoanzia Kibaha Maili Moja – Tumbi inakuja kutokea mpaka Mlandizi na kusonga mbele. Hilo ni la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, tunashirikiana vyema na wenzetu wa Jeshi la Polisi, tumeweka vikosi maalumu kabisa, kwa sababu barabara hii changamoto yake kubwa ni gari zinapoharibika ambazo zinaleta msongamano mkubwa. Kwa hiyo, vikosi vyetu vya TANROADS na Polisi vinashirikiana kwa pamoja, na hivi sasa kila linapotokea tatizo la namna hiyo, mara moja vikosi vile vinafanyia kazi na kuondoa lile gari lililoharibika na hatimaye kuruhusu barabara kuweza kupita.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kuhusu ni lini tutafanya sasa kazi ile ya Barabara ya Kibaha – Chalinze – Morogoro Express Way, tunashukuru sana kwa miongozo mikubwa na mizuri ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hivi ninavyokwambia tulichelewa hatua ya kwanza kwa sababu ya mkandarasi ambaye tuliingianaye katika mazungumzo, terms zake zilionekana kuwa hazina maslahi mapana kwa Taifa letu. Kwa hiyo, tumetangaza upya, na habari njema ni kwamba tumepata mpaka mashirika yetu ya ndani ikiwemo NSSF, TPA, walioonesha nia ya kuingia katika mradi huu mkubwa wa kielelezo na wa kimkakati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, timu za wataalamu wa Serikali, wako kazini wakichambua ikiwa ni pamoja na haya mashirika ya nje. Muda siyo mrefu tutakuwa tumepata atayekwenda kutekeleza kazi ile.

Name

Cornel Lucas Magembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato Kaskazini

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: - Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umefikia katika hatua gani?

Supplementary Question 2

MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Spika, kwanza ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza lenye sehemu (a) na (b). Kwanza ninapenda kujua Barabara ya kutoka Nyamirembe – Ichwankima – Kasenga – Biharamulo yenye zaidi ya kilometa 50, itaanza kujengwa lini, kwa sababu imekuwa ikiwekwa kwenye mpango wa ujenzi, lakini utekelezaji wake umekuwa haufanyiki?

Mheshimiwa Spika, la pili, ...

SPIKA: Ah, ah, swali ni moja tu.

MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tayari ameshafika ofisini kwa ajili ya kuulizia hiyo barabara. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tulishafanya usanifu, na katika mwaka wa fedha uliopita ilikuwepo kwenye bajeti. Nimhakikishie kwamba barabara hii tutaiweka kwenye bajeti kwa ajili ya kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami, kwa sababu tayari pia wenzetu wa uchukuzi wameshajenga bandari pale Nyamirembe ambayo sasa bila hiyo barabara itakuwa haina maana.

Name

Ibrahim Mohamed Shayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: - Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umefikia katika hatua gani?

Supplementary Question 3

MHE. IBRAHIM M. SHAYO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Ninaomba niulize swali la nyongeza. Je, ni lini Barabara ya Maili Sita – Kiboriloni ujenzi wa njia nne utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kuianza hiyo barabara, kwa sababu ni barabara ambayo inaanzia Tengeru inakwenda Kikafu – Maili Moja – Kiboriloni kwa njia nne. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tuko kwenye hatua za mwisho kabisa ili barabara hiyo ianze kujengwa. (Makofi)

Name

Nuru Issa Kashakari

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: - Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umefikia katika hatua gani?

Supplementary Question 4

MHE. NURU I. KASHAKARI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninaomba kuuliza swali la nyongeza linalohusiana na lini Serikali itajenga Daraja la Mto Malagarasi kule Ilagala? Pia ni lini Serikali itajenga Barabara kutoka Simbo – Kalya ili kuwanusuru wananchi wa Sunuka, Herembe, Mwakizega, na Buhingu?

Mheshimiwa Spika, barabara hii ni muhimu sana kwa sababu pale tuna Hifadhi ya Mahale, kwa hiyo, inasababisha watalii kupata usumbufu mkubwa sana. Kwa hiyo, ninaomba jibu kwa Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Daraja la Malagarasi maarufu kama Malagarasi Chini ambalo liko kwenye Barabara ya Simbo – Ilagala – Kalya ni daraja ambalo tumeshakamilisha usanifu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba pale ambapo daraja lipo, tutalihamisha, tutalipandisha kwa juu. Tumeshakamilisha usanifu, tupo tunaendelea na mazungumzo na wenzetu wa World Bank kupitia utaratibu wa CRW ili tuweze kulijenga daraja hilo. (Makofi)