Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 2 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 28 | 2026-01-28 |
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: -
Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umefikia katika hatua gani?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya kutoka Kibaha Maili Moja hadi Chalinze umegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya kutoka Maili Moja – Picha ya Ndege yenye urefu wa kilometa 3.6 kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya upanuzi wa sehemu hiyo ipo katika hatua za mwisho. Usanifu utakapokamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
Mheshimiwa Spika, sehemu iliyobaki ya kutoka Picha ya Ndege – Chalinze yenye urefu wa kilometa 78.9 itatekelezwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP). Kwa sasa taratibu za manunuzi ya kumpata mbia zinaendelea.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved