Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Edwin Malleko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha fedha za TASAF zinawafikia walengwa?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa TASAF imelenga kuwasaidia kaya maskini katika kupunguza umaskini katika hizo kaya, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba inawapatia wale watoto waliotoka kwenye kaya maskini mkopo wa elimu ya juu 100% ili na wao waweze kupata masomo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Ni namna gani bora mnayoitumia kwenye zile ajira zenu za muda, kwa sababu tumeona mara nyingi wanaoenda kufanya hizo kazi ni wazee na hawawezi kuzifanya kwa ufanisi? Mnafanya namna gani kuweza kuwapata ambao wanaenda kuzifanya hizo kazi za muda?
Name
Regina Ndege Qwaray
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mazuri. Swali lake la kwanza, Serikali kupitia TASAF imeweka mkakati wa kuhakikisha watoto wanaotoka katika kaya maskini wanapewa kipaumbele kwa maana wanapewa mikopo kwa 100%, na kwa utaratibu huo TASAF imefanya makubaliano na imesaini hati ya makubaliano kati ya TASAF pamoja na Bodi ya Mikopo ili kuhakikisha kwamba wale watoto wanapewa kipaumbele. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupitia hati ya makubaliano, TASAF imeendelea kuwapa kipaumbele wale watoto ambao wanatoka katika kaya maskini ili Bodi ya Mikopo iendelee kuwaona na kuwazingatia ili waweze kupata mikopo kwa 100%. Kupitia katika makubaliano hayo, TASAF pamoja na Bodi ya Mikopo imesaini makubaliano na katika makubaliano hayo, wamekubaliana na kuunganisha taarifa zao ili taarifa za TASAF ziunganishwe pamoja na taarifa ya Bodi ya Mikopo ili Bodi ya Mikopo waweze kuwapata kirahisi hawa watoto ambao wanatoka katika kaya maskini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia hilo, taarifa ni kwamba, mwaka wa fedha 2025/2026 takribani watoto 5,958 wameweza kupata mikopo ya elimu ya juu, jumla ikifikia watoto 18,000 wameweza kufanikiwa kupata mikopo ya elimu ya juu ili waweze kuendelea na masomo.
Mheshimiwa Spika, swali la pili kuhusu kazi au ajira za muda. Serikali kwa kupitia TASAF imeweza kuweka mkakati mzuri namna ya kutoa ajira za muda kwa walengwa, hasa wale ambao tayari wako kwenye mfumo, na kwa kupitia hivyo, Serikali imeendelea kusisitiza walengwa ambao tayari wameshasajiliwa katika kaya maskini waweze kupata kazi hizo za kujitolea au kazi za ajira za muda na hizi zinazotolewa ni mpango shiriki, kwamba jamii husika inashirikishwa ili kuwapata walengwa haswa ambao tayari wameshasajiliwa kwenye mfumo na tayari wanapatikana katika kaya maskini waweze kufanya kazi zile za ajira za muda.
Mheshimiwa Spika, kwa kupitia huko TASAF imeweka vigezo ambavyo vinatumika ili kuwapata wale washiriki. Kigezo mojawapo ni kuhakikisha kwamba washiriki wazingatie umri kuanzia miaka 18 mpaka 65, lakini kwa kuzingatia pia washiriki wale wanaoshiriki katika ajira za muda wawe na uwezo wa kufanya kazi kwa maana ya kuwa na afya njema na kigezo kingine ni kuhakikisha kwamba, wale washiriki ni wale ambao tayari waliosajiliwa kwenye mpango wa TASAF, ahsante. (Makofi)
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha fedha za TASAF zinawafikia walengwa?
Supplementary Question 2
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itazindua mpango wa tatu wa kaya maskini?
SPIKA: Hebu rudia tena swali lako.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, je ni lini Serikali itazindua mpango wa awamu ya tatu wa kaya maskini?
Name
Regina Ndege Qwaray
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali kwa sasa tayari imeshaweka mkakati wa kwenda kuanzisha mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu baada ya kukamilisha ule mpango wa awamu ya pili.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, mpango wetu wa awamu ya tatu ni kuhakikisha kwamba, tunaenda kuangalia yale mafanikio yaliyopatikana kwenye mpango wa utekelezaji awamu ya pili, lakini kuangalia changamoto iliyojitokeza kwenye awamu ya pili na kuenda kutafutia ufumbuzi.
Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Serikali iko kwenye maandalizi ya kutekeleza kuanzishwa kwa awamu ya tatu ya mpango, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved