Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fadhili Fabian Ngajilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. FADHILI F. NGAJILO aliuliza:- Je, lini Daraja la Isakalilo – Kitwiru litajengwa, ili kufungua Utalii wa Mbuga ya Wanyama Ruaha?
Supplementary Question 1
MHE. FADHILI F. NGAJILO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri kwa sababu, daraja hilo, wananchi wamekuwa wakiahidiwa muda mrefu zaidi ya miaka 20 iliyopita na sasa Serikali imetoa kauli yake. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, moja, nataka kujua, na wananchi wa Iringa Mjini wanataka kufahamu vizuri, ni lini hasa sasa mradi huu utaenda kukamilishwa na fedha zitatoka?
Mheshimiwa Spika, pili, wananchi wanataka kujua je, mradi huu utatekelezwa kama full package? Kwamba, daraja la mita 40 pamoja na kipande cha lami cha kilomita tatu, kama alivyopendekeza msanifu?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, kwenye huu Mradi wa TACTIC, Awamu ya Pili, ndani ya Manispaa ya Iringa Mjini, Serikali haina tatizo la fedha. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan ametenga shilingi bilioni 20, kwa ajili ya huu Mradi wa TACTIC.
Mheshimiwa Spika, mradi huu tunautekeleza kwa awamu mbili, kama nilivyoeleza. Tayari tumeshaanza awamu ya kwanza kwa kujenga Soko la Kihesa, kujenga barabara za Mkimbizi – Bima, Mtwivila, Viziwi na Bontank.
Mheshimiwa Spika, awamu ya pili ndiyo ujenzi wa daraja hili, pamoja na barabara za maingilio kwenye daraja hilo. Siyo hivyo tu, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Mradi wa RISE kwenye hii Manispaa ya Iringa Mjini anajenga barabara kwa kiwango cha lami, kilomita 37, kutoka Ipogolo kwenda Kilolo. Mradi huu tunautekeleza kwa pamoja na wenzetu wa TANROADS.
Name
Dr. Wilson Charles Mahera
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Primary Question
MHE. FADHILI F. NGAJILO aliuliza:- Je, lini Daraja la Isakalilo – Kitwiru litajengwa, ili kufungua Utalii wa Mbuga ya Wanyama Ruaha?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHARLES W. MAHERA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya Busegwe – Kitaramanka, yenye urefu wa kilomita 18 inapita katika kata tano za Busegwe – Mliaza – Buhemba na Mirwa, pamoja na Sirorisimba. Barabara hii ni muhimu sana kwenye shughuli za kiuchumi katika Jimbo la Butiama.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais alipokuja Butiama tulimwomba aweze kuipatia lami barabara hii akaridhia na kwa umuhimu wa barabara hii, ni Barabara ya TARURA, lakini inasimamiwa na TANROAD. Sasa swali la msingi, je, ni lini usanifu utaanza wa barabara hii, ili kusudi tuweze kupata lami katika Jimbo la Butiama?
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, ahadi za viongozi wetu wakuu wa nchi na hususan Mheshimiwa Rais, ni maelekezo kwetu sisi wasaidizi wake ndani ya Serikali. Namwahidi Mheshimiwa Mbunge Mahera kwamba, tunaendelea na utaratibu wa kupitia ahadi zote za viongozi wetu wakuu kwa nchi nzima na tumekuwa tukitekeleza kwa kadiri ambavyo fedha zinapatikana.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. FADHILI F. NGAJILO aliuliza:- Je, lini Daraja la Isakalilo – Kitwiru litajengwa, ili kufungua Utalii wa Mbuga ya Wanyama Ruaha?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Daraja la Ipanzya – Isalalo limekuwa ni kero ya muda mrefu sana. Ni lini Serikali itaanza kulijenga daraja hilo?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa RISE, tunajenga madaraja kwenye halmashauri 130 nchi nzima. Awamu ijayo na kadiri fedha zitakavyokuwa zinapatikana tutatenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved