Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 21 2026-01-28

Name

Fadhili Fabian Ngajilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. FADHILI F. NGAJILO aliuliza:-

Je, lini Daraja la Isakalilo – Kitwiru litajengwa, ili kufungua Utalii wa Mbuga ya Wanyama Ruaha?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, Fadhili Fabian Ngajilo, Mbunge wa Iringa Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Daraja la Isakalilo – Kitwiru lipo katika Barabara ya Isakalilo – Kitwiru yenye urefu wa kilomita tatu, ambayo inaunganisha kati ya Barabara ya TANZAM na Iringa kwenda Msembe. Daraja hili ni kiunganishi muhimu kuifikia Mbuga ya Wanyama ya Ruaha.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi wa TACTIC, Awamu ya Pili, imefanya usanifu wa mradi. Baada ya kukamilika kwa usanifu, mradi huu unaojumuisha ujenzi wa daraja pamoja na barabara za maingilio zenye urefu wa kilomita taru utaanza kutekelezwa.