Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: - Je, upi mpango wa kupunguza tozo kwa wakulima wa tumbaku, kwani kwa kila mfuko wa mbolea, benki hukata USD 0.5 na Benki Kuu USD 5.80?

Supplementary Question 1

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa nini sasa Serikali isikae na wadau wote wa sekta ndogo ya tumbaku pamoja na taasisi zote za fedha ili kubaini haraka changamoto ambazo zinaonekana kuongeza gharama za uzalishaji kwa mkulima ili kupunguza gharama?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa kuwa bei ya pembejeo ilipangwa kabla bei ya tumbaku haijatoka na walitumia grant list ya mwaka 2025 ambayo ilikuwa dola 2.1, lakini pia sasa bei ya tumbaku imeshuka na kuwa dola 1.5, Serikali haioni sasa kwamba wakulima hawa wanaenda kupata hasara na kusababisha kuuvuruga ushirika?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Ushetu na mdau mkubwa wa zao la tumbaku. Moja, amekuwa mtetezi mkubwa wa zao hili, lakini amekuwa akilisemea. Jambo moja ambalo nikuthibitishie ni kwamba Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na bahati nzuri hata Waziri wangu yupo hapa ananisikia, moja ya maelekezo ambayo Rais alitupatia ni kuwa wadau wanahitaji kukaa kikao na sisi ili kufanya mapitio na kuangalia namna bora ambayo tunaweza tukafanya maboresho tunaweza tukafanya kikao hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe tu shaka kwamba Serikali ipo tayari muda wowote kukaa na wadau, mabenki na sekta binafsi ili kuhakikisha kwamba tunafanya maboresho sahihi ambayo yanaweza kumsaidia mkulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bei ya tumbaku, moja wewe mwenyewe unafahamu kwamba bei ya tumbaku huwa inapangwa kwa kuangalia gharama za uzalishaji, hiyo ndiyo tunasema baseline. Ndiyo mahali ambapo huwa tunaanzia, halafu tukishaangalia zile gharama ndiyo tunatengeneza bei ambayo inaweza kumsaidia mkulima kupata faida. Kwa hiyo, bei ya mwaka huu baada ya kuzingatia vigezo vyote ndiyo ikaangukia katika dola 1.95.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge aliyoyasema, bado Serikali tunaweza tukaangalia na kuona namna bora ambayo tunaweza tukampatia faida zaidi mkulima hapa nchini, ahsante sana.