Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 8 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 86 2026-04-14

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: -

Je, upi mpango wa kupunguza tozo kwa wakulima wa tumbaku, kwani kwa kila mfuko wa mbolea, benki hukata USD 0.5 na Benki Kuu USD 5.80?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha kilimo cha zao la tumbaku ili kuongeza uzalishaji na tija kwa mkulima kwa kuimarisha mapato ya mkulima na kupunguza gharama za uzalishaji wa zao hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa, Serikali ipo kwenye hatua ya kupitia gharama za uzalishaji za mkulima ili kuainisha maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa maboresho ikiwemo riba za kibenki ambayo ni dola za Kimarekani 0.5 kwa mfuko wa mbolea ikiwa ni ada ya hati ya dhamana ya benki iliyotoa mkopo pamoja na dola za Kimarekani 5.8 inayojumuisha riba ya mkopo, dhamana ya Benki Kuu, bima ya mkopo na kodi ya ongezeko la thamani. Aidha, jitihada hizo zitaenda sambamba na kushirikisha Benki zinazotoa mikopo hiyo kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Bodi ya Tumbaku na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, zitaendelea na jitihada za kuboresha mazingira ya uzalishaji kwa wakulima wa zao la tumbaku ikiwemo kuboresha tija na kuainisha tozo ambazo zinahitaji kufanyiwa maboresho ili kuweza kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima wa zao hilo.