Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Moses Ludovico Kaegele

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. MOSES L. KAEGELE aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza ardhi kwa wananchi wa Vijiji vya Kasapa, King’ombe, Mlambo, Kala na Ng’undwe kutoka Hifadhi ya Lwafi kwa ajili ya kilimo?

Supplementary Question 1

MHE. MOSES L. KAEGELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaipongeza Serikali kwa majibu ambayo yana matumaini, lakini nina swali moja la nyongeza. Katika vijiji hivyo yapo maeneo ambayo yapo nje ya Hifadhi ya Loasi ya mipaka ya Hifadhi ya Loasi halali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado maeneo hayo yanaendelea kulindwa na watu wa hifadhi; na kwa kuwa wananchi wanaongezeka, lakini ardhi haiongezeki, je, Serikali haioni ni muda mwafaka basi wa kwenda kuangalia hiyo mipaka ili yale maeneo ambayo yapo nje ya hifadhi yaweze kurejeshwa kwa wananchi waweze kujiandaa na msimu wa kilimo ujao kwa ajili ya kuwaepusha na migogoro mingine ambayo inaweza kutokea? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu swali la Ndugu yangu Mheshimiwa Kaegele, kwanza ninampongeza sana kwa namna anavyowapambania wananchi wake hasa katika suala hili. Ni mara kadhaa anakuja ofisini, tunakaa kuzungumzia jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Serikali imepokea ushauri wake na ipo tayari kupeleka wataalamu wake kushirikiana na Halmashauri pamoja na Ofisi ya Mbunge ili kwenda kuhakiki mipaka hii na kutoa ufafanuzi unaofaa kwa maendeleo na maslahi ya wananchi.