Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 7 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 72 | 2026-04-13 |
Name
Moses Ludovico Kaegele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. MOSES L. KAEGELE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaongeza ardhi kwa wananchi wa Vijiji vya Kasapa, King’ombe, Mlambo, Kala na Ng’undwe kutoka Hifadhi ya Lwafi kwa ajili ya kilimo?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Hifadhi ya Msitu Loasi ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na. 346 la 25/10/ 1957 ikiwa na ukubwa wa hekta 33,468. Msitu huu unazungukwa na vijiji vinne ambavyo ni King’ombe, Mlambo, Kilambo Mkorochi na Mpasa. Vijiji hivyo vilibainika kuvamia sehemu ya hifadhi kwa matumizi mbalimbali ya kijamii ambapo Baraza la Mawaziri kupitia Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta lilielelekeza Serikali kumega hifadhi ili kupata suluhu ya migogoro hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, mwaka 2023 Serikali ilitekeleza Maelekezo hayo kwa kumega eneo lenye ukubwa wa hekta 10,834 (sawa na ekari 27,050) kutoka kwenye hifadhi na kugawiwa kwenye vijiji kulingana na mahitaji yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali haioni haja ya kuendelea kumega eneo la hifadhi kutokana na umuhimu wake wa kiikolojia na kijamii. Hii inatokana na ukweli kwamba hifadhi hii ni chanzo kikuu cha maji ya Mto Loasi na Msalamba. Hali kadhalika, inahifadhi mimea na Wanyama, inasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuepusha migogoro ya wanyama wakali na waharibifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande mwingine maji yanayotiririka kutoka hifadhi hii huchangia katika maporomoko maarufu ya Kalambo (Kalambo Water Falls) ambayo huchochea utalii na uchumi wa nchi katika ukanda huo. Aidha, Serikali inaendelea kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za uhifadhi na kutumia hifadhi kwa shughuli rafiki za kimazingira kama ufugaji nyuki ili kujipatia kipato endelevu.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved