Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Faraji Buriani Nandala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 1

MHE. FARAJI B. NANDALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati. Nina maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya eananchi wa Jimbo la Ndanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya mwaka 2025/2026 ndiyo hii ambayo tunaitekeleza na tunaelekea kuikamilisha hivi karibuni. Hizi fedha shilingi bilioni tano zilishatengwa, ina maana zipo. Kwa hiyo, nataka majibu ya Serikali, ni lini hasa watawalipa hawa wananchi wakati tuko kwenye process za kupitisha bajeti mpya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ninataka kufapata ushauri wa Serikali, je, wale wananchi waendelee kuandaa mashamba yao au wasiendelee, kwa sababu hii gridi ya Taifa inapita kwenye mashamba ya wananchi? Kama wasiandae yale mashamba, je, Serikali itakuwa tayari kulipa penati itayotokana na kuchelewesha kulipwa kwa hii fidia yao?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninampongeza sana kaka yangu Mheshimiwa Faraji kwa kufuatilia maslahi ya wananchi wake wa Ndanda, amekuwa anatufuatilia mara kwa mara na kuja ofisini kwa ajili ya kujua hatima ya line hii ambayo itaingiza mikoa ya Lindi na Mtwara katika gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa, sisi Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Fedha, tunajitahidi sana kuhakikisha kwamba fidia italipwa kwa wakati ili wananchi hawa wasiingie kwenye mgogoro mwingine kati yao na Serikali. Kwa hiyo, hilo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunajitahidi kutafuta fedha, na bado muda tunao, na hilo litatendeka ndani ya mwaka huu wa fedha, Mwenyezi Mungu akitujalia.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 2

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni takribani miaka miwili inaenda mitatu sasa tangu Wananchi wa Kipagalo – Bulongwa - Iniho wapishe mradi wa Bwawa la Umeme la Lumakyala lakini Serikali haijatoa kauli ni ipi jibu la Serikali kwa wananchi hawa ili waweze kupata fedha zao kutokana na tathimini iliyofanyika?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, utaungana nami kukubaliana kwamba Mheshimiwa Sanga amekuwa ni Mheshimiwa Mbunge kinara katika kufuatilia maslahi ya wananchi wake wa Jimbo la Makete. Nimhakikishie, hili bwawa la umeme litazalisha Megawati 222, na ni la muhimu sana katika kuchangia megawati 8000 ambazo ndiyo lengo la Serikali kwa mwaka huu mpaka 2030.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatafuta fedha kupitia TENESCO na TANESCO ipo katika mazungumzo na wabia mbalimbali ili tuweze kujenga mradi huu kwa PPP. Wananchi wake watalipwa fidia na tutajenga bwawa hili na tutafikia adhima yetu ya kuzalisha umeme ya Megawati 222.

Name

Emanuel Qambaji Nuwas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Mji Mdogo wa Haydom ambao unategemea umeme kutoka Mji wa Katesh ambapo umeme huo hupita umbali mrefu sana na hivyo Mji huu kupata changamoto ya umeme kukatikatika mara nyingi, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kituo cha kupoozea umeme ili kuwahakikishia wananchi hao kupata umeme wa uhakika?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la Serikali siyo tu kuhakikisha taa zinawaka, lakini pia ni kuhakikisha nishati ya umeme inatumika kwa ajili ya uchumi. Kwa sababu hiyo, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba wananchi wanapata umeme wa kutosha ambao utawasidia katika kuendesha maisha yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mheshimiwa Mbunge nimelipokea, tutajenga substation katika eneo hili ili kuimarisha upatikanaji wa umeme ambao unaweza kusaidia katika uchumi wa eneo lake. Ahsante.

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 4

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza ninaishukuru Serikali kwa mpango wa kuweka Mkoa wetu wa Kagera kwenye gridi ya Taifa, na katika mipango hii wananchi wa Kata za Nyakahanga, Kata ya Bugene na Kata ya Kayanga wamepisha ujenzi wa gridi ya Taifa, lakini hawajapata fidia. Je, ni lini watalipwa fidia?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninampongeza Mheshimiwa Innocent Bashungwa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuzungumza na wananchi wake ili waweze kuridhia kupisha mradi wa line ya umeme katika eneo hilo ambalo kimsingi kama alivyosema, litatusaidia kuunganisha Mkoa wa Kagera katika katika gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mpaka sasa tumeshalipa shilingi milioni 385 ili kuweza kujenga substation, lakini tutakwenda kulipa shilingi bilioni 5.8 kwa wananchi zaidi ya 1,001 ambao wao wameridhia kupisha ujenzi wa line ambayo itasafirisha umeme kwenda katika Mkoa wa Kagera. Ahsante.

Name

Marirta Gido Kivunge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 5

MHE. MARIRTA G. KIVUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Je, ni Serikali itakamilisha zoezi la kufikisha umeme kwenye vitongoji vilivyosalia katika Wilaya ya Longido na hasa kwenye vyanzo vya maji?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 vitongoji vyote ndani ya nchi yetu vinapata umeme. Nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Serikali tutafika kwenu na tutakapopata fedha, tutahakikisha kwamba vitongoji hivyo alivyovitaja vianapata umeme na Mheshimiwa Mbunge atakuwa ni sehemu ya watu ambao tutakwenda kuzindua kuwasha umeme kwenye vitongoji hivyo. Ahsante.

Name

Tinnar Andrew Chenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 6

MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kumekuwa na changamoto ya kukatikakatika umeme katika Mkoa wa Simiyu, na Serikali iliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kujenga kituo cha kupozea umeme. Je, ujenzi huu umefikia hatua gani? Lini utakamilika ili kuondoa changamoto hii? (Makofi)

Name

Salome Wyckiffe Makamba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia namna ambavyo Wizara ya Nishati inaendelea kutekeleza majukumu ya ujenzi wa substation katika eneo la Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi inaendelea na mpaka sasa ujenzi wa substation umefika zaidi ya 30%. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira. Ninamhakikishia mara baada ya substation hiyo kukamilika, Mkoa wa Simiyu utakuwa umeondokana na changamoto ya kukatikakatika kwa umeme. Ahsante.

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: - Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?

Supplementary Question 7

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa nafasi. Wananchi wa Jimbo la Missenyi walipisha ujenzi wa Mradi wa Kakono ambao unaleta umeme katika substation ya Kyaka. Sasa hivi ni takribani miaka mitatu, na mwaka 2025 tathmini ilifanyika, wanadai shilingi bilioni 1.5, lakini mpaka leo hawajalipwa. Je, ni lini sasa wananchi hao watalipwa ili waweze kuendelea na maisha yao mengine na kupisha mradi uendelee?

Name

Salome Wycliffe Makamba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza pia Mheshimiwa Mbunge kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wake hata waliridhia kupisha mradi huu wa kujenga Substation ya Kakono. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutakwenda kulipa fidia kwa wananchi hawa kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kwa kadiri fedha ambavyo itapatikana.