Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
John Stephano Luhende
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa katika eneo la Kisasiga Jimbo la Bukene?
Supplementary Question 1
MHE. JOHN S. LUHENDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi nyingine ya maswali ya nyongeza. Swali langu la kwanza la nyongeza, ninataka kuuliza mradi wa umwagiliaji wa Kata ya Sigili, Vijiji vya Iyalemwalagwa na Bulambuka umefikia 39%; na mradi huu umeanza kujengwa tangu 2023, wastani sasa wa chini ya 10% kila mwaka.
(a) Je, ni lini wataweza kuukamilisha mradi huu ili uweze kuwasaidia wananchi katika shughuli za kilimo?
(b) Je, ni lini mtaanza ukarabati wa bwawa lililopo Kata ya Kahama ya Haranga, ili liendelee kusaidia wananchi walioko huko katika shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mheshimiwa Luhende, Mbunge wa Jimbo la Bukene kwa maswali yake ya msingi. Nimthibitishie tu jambo moja, kwamba miradi yote ambayo inatekelezwa katika eneo la jimbo lake na maeneo mengine yote nchini, Serikali tulishaiweka katika mipango. Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba inakamilika kwa wakati. Kwa hiyo, hata hili Bwawa la Bulambuka ambalo amesema ni lini litakamilika, niseme litakamilika kulingana na mkataba ambao tulikuwa tumeandikishana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba muda ulizidi kwa sababu kulikuwa na changamoto ya kifedha. Sasa hivi Wizara ya Fedha imeji-commit kutoa fedha kila mwezi ambazo zitasaidia sisi kuwalipa wale wakandarasi ili waweze kukamilisha ile miradi kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jibu hilo la kwanza ndilo linaloambatana na vilevile katika mradi wa Bwawa la Kahama Mlanga, kwamba kwa sababu sasa tuna uhakika kwamba tutakuwa na flow nzuri ya kupata fedha, maana yake miradi hii sasa tutakuwa tuna uwezo wa kuipelekea fedha na kukamilika kama vile ambavyo imepangwa.
Name
Fadhili Fabian Ngajilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa katika eneo la Kisasiga Jimbo la Bukene?
Supplementary Question 2
MHE. FADHILI F. NGAJILO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la msingi linahusu skimu za umwagiliaji. Pale Iringa Mjini kuna skimu ya umwagiliaji ya wenyeji inayojulikana kwa jina la Mkoga Chelahani inapatikana Kata ya Isakalilo. Hii skimu imeajiri watu wengi sana zaidi ya 10,000 ambao wanaitegemea. Sasa swali, je, Serikali iko tayari kuijenga upya, kuiboresha ili iweze kutoa ajira zaidi kwa wananchi wa Iringa? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Vilevile ninamshukuru Mbunge wa Iringa Mjini, Bwana Fadhili Ngajilo na nimwondoe shaka tu, aende akawathibitishie tu wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini kwamba, Serikali tuko tayari kufanya ukarabati na kuboresha skimu hiyo ili kuhakikisha kwamba inaleta tija kwa wananchi wale.
Name
Rashid Mohamed Mtima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Newala Mjni
Primary Question
MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa katika eneo la Kisasiga Jimbo la Bukene?
Supplementary Question 3
MHE. RASHID M. MTIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza swali la nyongeza katika sekta hii ya kilimo kwamba, ni lini Serikali itakamilisha designing ya mradi wa umwagiliaji eneo la Chikwedu, Chipalang’anda na Lipeleng’inyi ambalo utawezesha wananchi wa Vijiji vya Chihanga, Mpilipili, Chiunjila na Tarafa ya Mkunya jumla, ili kutumia maji ya Mto Ruvuma kuweza kumwagilia na kuongeza kipato kupitia sekta hii ya uzalishaji ya Kilimo? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu katika maswali niliyotangulia, ni kwamba miradi yote ya umwagiliaji ikiwemo hii ambayo ameitaja Chipalang’anda, (majina yake ni magumu kidogo), lakini miradi yote hii sisi kama Serikali tulishapewa maagizo na Mheshimiwa Rais kuingiza katika mipango, kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili tupate gharama halisi, na baada ya hapo tuweze kuitangaza ili iweze kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, at least kwenye suala la miradi ya umwagiliaji, kwa sababu ni ajenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita, niseme tu kwamba haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais, na sisi jukumu letu ni kutekeleza. Kwa hiyo nimwondoe tu shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba tunalifahamu, na kazi inaendelea.
Name
Japhael Masanja Lufungija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulyankulu
Primary Question
MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa katika eneo la Kisasiga Jimbo la Bukene?
Supplementary Question 4
MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Napenda kumwuliza Naibu Waziri kwamba, Jimbo la Ulyankulu kuna mradi wa bwawa la umwagiliaji pale Kata Konanne, ambapo Serikali imeahidi kwa muda mrefu kulijenga, lakini pamoja na Bwawa la Mwamnange, je, ni lini utekelezaji wa miradi hii utaanza kufanyika?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika miradi ambayo Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, tumepanga kuitekeleza kuanzia mwaka wa fedha unaokuja ni pamoja na ambayo baadhi ameitaja Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, matarajio ni kwamba sasa tunakwenda katika utekelezaji baada ya kukamilisha upembuzi na usanifu wa kina.
Name
Azza Hilal Hamad
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOHN S. LUHENDE aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha kisasa katika eneo la Kisasiga Jimbo la Bukene?
Supplementary Question 5
MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji katika skimu ya umwagiliaji ya Masengwa iliyopo katika Jimbo la Itwangi? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninarudia tena kwamba miradi mingi ya umwagiliaji ambayo Wizara ya Kilimo tunaitekeleza ipo katika hatua mbalimbali. Ipo ambayo tunaifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili tuweze kupata gharama halisi na kujua design za michoro ili tuweze kuitekeleza. Vilevile, ipo ambayo tumeshatangaza kwa ajili ya kupata wakandarasi na ipo ambayo inaendelea kwa maana wakandarasi wako kazini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukiwemo huu wa mradi wa Masengwa katika Jimbo la Itwangi ni sehemu ya miradi ambayo tunamalizia upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunapeleka fedha ili sasa uanze kufanya kazi na wananchi waweze kupata huduma hiyo ya umwagiliaji.