Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawili. Ninaomba niipongeze Serikali kwa majibu mazuri, lakini pia nipongeze kwa ujenzi wa kiwango cha barabara ya kutoka Ipogolo – Idete. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Kilolo na barabara hii inaunganisha kata nyingi ikiwepo Makao Makuu ya Kilolo, Kata za Mtitu, Kising’a, Upwega, Udekwa, na Ilula. Barabara hii inaunganisha kata zilizopo eneo la chini na eneo la juu katika Jimbo letu la Kilolo na ina Daraja la Lukosi. Daraja hili limeanza kujengwa tangu tarehe 15 Februari, 2023. Tulitegemea suluhisho la daraja hili lingeweza kusaidia, kwa sababu sasa hivi kuna vidaraja vidogo ambavyo havipitiki, ule mto ukiwa umejaa maji: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini daraja hili litakamilika ili wananchi wa Kilolo wasiendelee kupata mateso makubwa ambayo wanayapata wakati wa mvua?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa kuwa barabara inayotoka Kibaoni inapita Ukumbi – Kitoo hadi Ihemi, Iringa DC, ni barabara ya kiuchumi mkubwa na inapitisha magari makubwa sana ya mbao; sasa kutokana na ubovu wa barabara hii magari yamekuwa yakikwepa njia ya kupita katika barabara hii na kwenda kupita kwenye halmashauri nyingine na kusababisha upotevu wa mapato makubwa katika Wilaya yetu ya Kilolo, je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuboresha hii barabara ili Kilolo iweze kupata mapato yao yote bila kwenda kupitisha kwenye halmashauri nyingine?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mheshimiwa Dkt. Ritta, Mbunge wa Kilolo kwa kuipongeza Serikali kwa kukamilisha kujenga barabara kutoka Ipogolo – Kilolo yenye urefu wa kilometa 33 kwa kiwango cha lami, tunamshukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, na hasa kuhusu daraja ambalo lipo katika barabara aliyoiuliza, ni kweli daraja hili ni muhimu sana kulijenga. Tayari tuna mkandarasi yupo site, lakini amechukua muda mrefu. Mkataba wake unamtaka kabla ya mwisho wa huu mwaka awe amekamilisha kulijenga daraja hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama Serikali tutahakikisha kwamba tunamlipa fedha hiyo, kwa sasa yupo site anafanya kazi, daraja lenye gharama ya kama shilingi bilioni 2.8 ili aweze kukamilisha na kuondoa adha ambayo inawakabili wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Barabara ya Kibaoni – Itoho – Ihemi, tumepokea. Ninapenda nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kupitia Bunge lako nimwagize Meneja wa Mkoa wa Iringa ahakikishe kwamba barabara hii inapitika muda wote ili wananchi wasiweze kupata adha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli barabara hizi ambazo ni changarawe kipindi cha mvua, na hasa eneo lake lina mvua nyingi sana, zinakuwa na changamoto. Hivyo, meneja ahakikishe kwamba hii barabara inapitika.

Name

Shaffin Ahmedali Sumar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uyui

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Ninaomba kuuliza swali. Je, ni lini barabara inayounganisha barabara tatu, kwa maana ya Tabora Mjini – Ulyankulu na Jimbo la Uyui, itajengwa kwa kiwango cha lami ambapo wananchi wengi wanahitaji lami ili waweze kunufaika na huduma hiyo?
MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani sijamsikia, amesema Tabora Mjini hadi...

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara inayoounganisha wilaya tatu za Tabora Mjini, Ulyankulu na Uyui ambapo kuna kata zangu za Idiri na Usagai.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii tumeshaifanyia usanifu, na kwa kweli Serikali inatafuta fedha ili iweze kuijenga kwa sababu ni kweli ni barabara muhimu na inapita kwenye maeneo mengi na hasa ikiwa inaunganisha hizo wilaya alizozitaja Mheshimiwa Mbunge. Tumeshakamilisha usanifu, kwa hiyo, Serikali inatafuta fedha ili kuijenga kwa kiwango cha lami.

Name

Issaay Zacharia Paulo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?

Supplementary Question 3

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Kwa kuwa ni takribani miaka mitatu sasa, Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani – Magara – Mbulu, usanifu wake ulishakamilika na ahadi nyingi za viongozi wetu wakuu zimetolewa kwa wananchi wa Jimbo la Mbulu Mjini. Je, ni lini barabara hii itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda sijamwelewa vizuri, ni Barabara ya Mbulu – Galbad!

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani – Magara – Mbulu, usanifu wake umekamilika kwa miaka miwili zaidi ya miaka miwili sasa. Ahadi nyingi za viongozi wa Kitaifa zimetolewa kwenye hii Barabara. Je, ni lini ujenzi wa barabara hii utaanza kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hii Barabara ya Mbulu – Mbuyu wa Mjerumani ni barabara ambayo inapita kwenye miinuko mikali sana. Ni kweli maelekezo ya viongozi wetu wa Kitaifa wameshatuelekeza tuijenge kwa kiwango cha lami. Tumeshakamilisha usanifu, lakini kitu cha kwanza ilikuwa ni kujenga kwanza daraja ambalo lilikuwa ni korofi, daraja la Magara ambalo tulishalikamilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, maeneo mengi korofi tulikuwa tunayajenga na bado tunaendelea kuyajenga kwa kiwango cha zege ili ziweze kupitika, na wakati hiyo tunatafuta fedha ili barabara hiyo tuweze kuijenga kwa kiwango cha lami.

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?

Supplementary Question 4

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa barabara ya Mwigumbi – Maswa inakarabatiwa angalau kila mwaka, mwaka 2024 imekarabatiwa, mwaka 2025 imekarabatiwa, na hata sasa vipande vingi vinakarabatiwa. Je, ni kwa nini Serikali isiifumue barabara hii yote kwa ujumla na kuijenga upya, kwa sababu inaonekana haikujengwa kwa ubora unaotakiwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge. Kilichofanyika Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi alishatoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS wa Mkoa, lakini pia na Meneja wa Makao Makuu waweze kwenda wakafanye tathmini na watoe taarifa ya kina ili Serikali ione inafanya nini kuhusu hiyo barabara ambayo imekuwa mara kwa mara inafanyiwa matengenezo wakati ni barabara ambayo haijajengwa muda mrefu.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali. Barabara ya kutoka Bulige - Kahama kupita Mwakitolyo – Solwa mpaka Salawi ni barabara muhimu sana. Je, ni lini itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii barabara inajengwa kwa kiwango cha lami kwa awamu. Ni kweli tumejenga kidogo kidogo, lakini tumeshakamilisha usanifu. Kwa sasa tunajenga kwa vipande wakati tunatafuta fedha ya kuikamilisha barabara yote.