Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 7 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 65 | 2026-04-13 |
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: -
Je, lini Barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula itakamilika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kilolo – Udekwa – Ilula ni barabara ya mkoa inayojulikana kwa jina la Kilolo – Ipalamwa – Watalisoli – Ilula yenye urefu wa kilometa 91. Kwa sasa, Serikali ipo katika hatua za mwisho za manunuzi ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved