Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sara Msafiri Ally

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi, na ninaipongeza Serikali kwa majibu mazuri na kwa mipango mizuri ya kuboresha barabara zetu hasa zilizopo chini ya TANROADS. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, barabara hii ni barabara ya kimkakati ya kiuchumi ambapo kuna shughuli za kiuchumi za uchimbaji wa madini, madini ambayo yanategemewa sana kwenye viwanda vya tiles, Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani na Kituo cha Afya kikubwa kinachotegemewa na Tarafa mbili ya Mlali na Mgeta, lakini kuna soko kubwa la kisasa pale, barabara hii imekuwa ikikwamisha shughuli za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni ipo haja sasa ya kutenga fedha kwa ajili ya kufanya feasibility study ili barabara hii ya kilometa 59 ijengwe kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa barabara hii imeenda mpaka ikaunganika na Kituo cha Kisaki cha Treni ya TAZARA na wananchi wa Tarafa ya Mgeta na Mlali ni wazalishaji wakubwa kama nilivyoongea kwenye swali la kwanza: Je, Serikali haioni kuchelewesha kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami ni kuwachelewesha wananchi kuboresha shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakubali kwamba barabara hii ni ya muhimu sana. Kama alivyosema, kwamba kuna shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo madini, kituo cha afya, lakini pia kuna soko. Ndiyo maana tumesema kwamba tunahakikisha inapitika muda wote, na yale maeneo ambayo yamekuwa yanakwamisha, tunayaboresha kwa kuyajengea lami ama zege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, katika jibu langu la msingi, tumekiri kwamba tunatafuta fedha ili tuweze kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, kuhusu kuunganisha na Kisaki, ninakiri kwamba hii barabara ndiyo inayounganisha hawa wananchi mpaka kituo cha TAZARA cha Kisaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna vipande viwili. Sisi Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tunaishia pale Kikeo na kutoka Kikeo kwenda Kisaki inahudumiwa na wenzetu wa TARURA. Kwa hiyo, tutawasiliana na wenzetu ili tuweze kuhakikisha kwamba, wakati hatujaijenga kwa kiwango cha lami, lakini barabara yote iweze kupitika kuanzia hapa ambapo inaanzia, Sangasasanga – Kikeo hadi Kisaki, ahsante.

Name

Edefonce Joackim Canoni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pia ninashukuru kwa kupata mradi wa barabara kutoka Matai – Kashesha ambayo ni ya kilometa 50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ikikamilika, itachochea uchumi sana katika Wilaya ya Kalambo, na Serikali itakusanya mapato katika Kituo cha Forodha Kashesha. Wananchi wa Kalambo wanataka kupata majibu ya Serikali, je, ni lini barabara hii ambayo inaendelea kusuasua, itakamilika ili waweze kufaidika? Watapata ajira, tutachochea Uchumi, na pia tutapata wawekezaji kwa sababu ipo mpakani mwa Zambia na Tanzania.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakiri kwamba hii barabara ni muhimu sana na hasa kwa kipindi hiki kwa sababu ni moja ya barabara kuu, na pia tuna kituo chetu cha forodha kule. Tunavyoongea barabara hiyo kutoka Matai – Kasese ina kilometa 50. Mheshimiwa Mbunge atakubalina, kwamba, ili kufanya haraka tumeigawa katika vipande viwili, kwa maana ya lots; Matai – Tatanda, Tatanda – Kasesya na tuna Wakandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tumechelewa kwa sababu mkandarasi alikuwa anadai. Tumeshamlipa na mkandarasi wa kipande cha pili tunafanya maandalizi ya kumlipa ili barabara hii iweze kukamilika, kwa sababu sasa magari mengi yanayotokea Zambia yanapita huko kwenda mikoa ya Kaskazini na hata kwenda nchi jirani. Kwa hiyo, tunalitambua hilo na tunalipa umuhimu mkubwa sana kuhakikisha kwamba hiyo barabara yote inajengwa kwa kiwango cha lami, ahsante.

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya kutoka Bariadi – Itilima – Meatu – Sibiti hadi Singida iko kwenye Ilani, je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara hii muhimu kwa vile ndiyo itakuwa shortcut?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli barabara hii iko kwenye kiwango cha lami, ilikuwa haijakamilishwa usanifu. Tunachokamilisha sasa hivi ni usanifu wa kina wa barabara hii ambayo ni muhimu sana kwa wenzetu wa Mkoa wa Simiyu. Baada ya hapo, tutatafuta fedha kwa ajili ya kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kibaya – Kisima kilometa 50 walisema wataijenga kwa kiwango cha lami. Kipindi hiki cha mvua wananchi wa Kiteto wamesumbuka sana. Je, ni lini barabara hii itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Ninakushukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, barabara hii ambayo ni ya kipande cha kutoka Handeni – Kibirashi – Kibaya kwenda kwa Mtoro kilometa 50 Kibaya – Kisima, tunachosubiri tu sasa hivi ni kumpa mkandarasi malipo ya awali ili aweze kukijenga kipande hicho cha kilometa 50.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkandarasi yupo tayari, tumeshapeleka maombi yetu Hazina ili aweze kulipwa malipo ya awali aanze kazi, ahsante.

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SARA M. ALLY aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kipera – Mlali – Nyandila – Luale – Kikeo hadi Kisaki kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 5

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kuniona. Manispaa ya Morogoro ni Manispaa ambayo barabara zake nyingi ni za vumbi, hazijaunganishwa kwa lami. Kwa mfano, Kata ya Mkundi, Bigwa, Kihonda, Tungi hazina lami. Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kuunganisha barabara hizi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nilipokee swali la Mheshimiwa Mbunge wa Morogoro, lakini niseme tutawasiliana na wenzetu wa TARURA kwa sababu barabara nyingi za mijini zinasimamiwa na wenzetu wa TAMISEMI kupitia TARURA. Hata hivyo, kama Serikali, tumelichukua na tutampa majibu sahihi.