Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Timotheo Paul Mnzava
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 1
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa sasa hivi hali ya wafugaji ya Mkoa wa Tanga ni mbaya. Kiwanda mnachosema kinao uwezo wa kusindika lita 120,000 kwa siku. Kwa uhalisia kwa sasa, kinasindika lita zisizozidi 20,000. Kiwanda hiki kinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo madeni makubwa, pia changamoto za kiuendeshaji. Kwa hali ilivyo, hatuoni matumaini ya hivi karibuni kutatua changamoto ya kiwanda hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali iko tayari kutafuta mpango mwingine wa kuvutia wawekezaji wengine tujenge kiwanda kingine cha maziwa kwa ajili ya kusaidia wafugaji wa Mkoa wa Tanga?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tunaipongeza Serikali kwa mradi huu mzuri wa mageuzi ya tasnia ya maziwa, lakini kiuhalisia, mradi huu sisi Korogwe Vijijini haufiki ambako uhitaji ni mkubwa sana ikiwemo uhitaji wa maeneo ya kuhifadhia maziwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali iko tayari wakati wa mapitio ya mradi huu, tuongeze na Wilaya ya Korogwe Vijijini iwe mnufaika wa mradi huu ili wafugaji wa Korogwe Vijijini waendelee kupata uhakika wa kuhifadhi maziwa yao na kupata bei ya kueleweka? (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Timotheo Mnzava kwa sababu amekuwa akifuatilia mgogoro huu kwa karibu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tulikaa kikao pamoja na Wabunge wote wa Mkoa wa Tanga. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana na kuwapongeza kwa kufuatilia maslahi mapana ya wafugaji wa Mkoa wa Tanga. Mwenyekiti wa kikao hiki alikuwa ni Mheshimiwa Timotheo Mnzava, ninawapongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba, moja ya vipaumbele vikubwa sana katika Wizara yetu kwa sasa ni pamoja na utatuzi wa changamoto zilizopo katika kiwanda hiki. Tunatambua ni kwa kiasi gani uimara wa kiwanda hiki ulikuwa unachangia katika kuongeza soko la maziwa na bei nzuri kwa wafugaji wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tumeshaanza kuchukua hatua. Tayari Waziri wa Mifugo na Uvuvi amekaa kikao na uongozi wa TADB ambao ni mdeni namba moja wa kiwanda hiki. Pia, tumeshakaa vikao na wadeni wengine, tumekaa kikao katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi alikwenda Tanga mahsusi kabisa katika kikao na wadau wote wanaohusika na changamoto katika kiwanda hiki ili kuona namna gani tunakwenda kuzitatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Wabunge wote wa Mkoa wa Tanga, wananchi wote wa Mkoa wa Tanga na wale wote wa Mikoa jirani ambao walikuwa wananufaika na kiwanda hiki, kwamba moja ya vipaumbele vyetu kwa sasa ni utatuzi wa changamoto katika kiwanda hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wakati huu, wakati tunaendelea na utatuzi wa changamoto za kiwanda hiki, tunaendelea na kuvutia pia wawekezaji binafsi ili waweze kutambua fursa zilizopo katika Mkoa wetu wa Tanga, ikiwemo wingi wa malighafi hii ya maziwa ili tuweze kuanzisha viwanda vingi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili, mradi huo ambao tunakwenda kuanzisha wa Mikoa Nane ambayo iko Kanda ya Ziwa na mitano Zanzibar, ni kweli, katika Mkoa wetu wa Tanga tunazo Wilaya tatu, Wilaya ya Lushoto, Muheza na Wilaya ya Mkinga na Wilaya ya Korogwe Vijijini ambazo kwa sasa katika mradi huu hazipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mbunge kwamba Serikali tunaendelea na juhudi mbalimbali za kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha hizi milk collection centres katika sehemu mbalimbali ambazo hatuna, ili kupunguza upotevu wa maziwa. Pia tunaendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ili tuweze kupata fedha za miradi mbalimbali na kule ambako hatuna hizi milk collection centres tuziweke.
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi nimpe tu uhakika kwamba Wilaya yetu ya Korogwe Vijijini itakuwa kipaumbele. (Makofi)
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nina swali kwa Waziri. Wananchi wa Jimbo la Ludewa wanapenda sana kufuga samaki Ziwa Nyasa ila kuna changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa vifaranga vya samaki ambavyo vinaendana na ekolojia ya Ziwa Nyasa. Je, Serikali iko tayari kuwezesha Kituo cha TAFIRI, Mbeya na Ruhila, Songea ili waongeze uzalishaji wa vifaranga vya samaki na kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha samaki kirahisi? (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kati ya maziwa yetu makuu ambayo tunayo hapa nchini, na sisi kama Wizara tunayaangalia kama maziwa ya mkakati, ni pamoja na Ziwa Nyasa. Tunaendelea kufanya mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kwamba vituo vyetu ambavyo vinazalisha vifaranga ambavyo ndiyo vina-supply kwa wote wanaofuga kwenye Ziwa Nyasa vinaongezewa uwezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kati ya fedha ambazo tumepokea sasa hivi Wizarani kwa ajili ya kuwezesha vijana kwenye uvuvi na mifugo, baadhi ya fedha hizo pia zitakwenda kuwawezesha vijana katika Ziwa Nyasa. Kwa hiyo, tunao mpango na mkakati wa kuhakikisha wale wote wanaowekeza katika Ziwa Nyasa wanapata chakula na vifaranga kwa wakati na kwa uhakika. Nakushukuru sana.
Name
Ramadhani Hamza Singano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 3
MHE. RAMADHANI H. SINGANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika mipango mizuri ni kuweka mipango ya muda mfupi ya kati na ya muda mrefu. Sasa kwa kuwa wananchi wa Tanga wameshahamasika sana na zao hili la maziwa, Serikali ina mpango gani wa muda mfupi wa kuhakikisha kwamba wananusuru mapato haya yanayopotea katika zao la maziwa? (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana. Nami ninampongeza sana Mbunge mwingine wa Mkoa wa Tanga ambao kwa kweli kwa kiasi kikubwa wanafuatilia mgogoro huu kwa karibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyozungumza katika swali la msingi, mgogoro huu ni kipaumbele chetu kwa sasa. Tunaendelea kutafuta solution za muda mrefu, lakini hata za muda mfupi ikiwa ni pamoja na kuona namna gani tunaweza kutenga fedha kadri zinavyopatikana kuongeza juhudi ya kuhakikisha tunazuia upotevu wa malighafi hii ya maziwa kwa wafugaji wetu wa Mkoa wa Tanga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kulifanyia kazi kwa karibu sana.
Name
Joshua Samwel Nassari
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 4
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kuniona. Swali la msingi limeulizia habari ya soko na bei ya maziwa kwa wafugaji. Sasa Katika kukabiliana na tatizo hilo la soko na bei, wakulima na wafugaji wa Meru wameanzisha umoja wao unaitwa UWAWAME (Umoja wa Wakulima na Wafugaji Meru). Wanachohitaji kwa Serikali ili waweze kusaidika ni kuongeza thamani kwenye mazao ya maziwa na vitu vingine. Kuna baadhi ya vitu ambavyo wanahitaji msaada kutoka kwa Serikali kwa maana ya Wizara inayohusika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali iko tayari basi kukutana na hawa UWAWAME ili waweze kuwasaidia waweze kukabiliana na hii changamoto ya bei na soko kwenye maziwa?
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ninamshukuru pia Mbunge kwa sababu mara kwa mara amekuwa akiniuliza juu ya namna gani tunaweza tukawafanya UWAWAME waweze kuendelea kuzalisha kwa tija zaidi hasa wafugaji katika umoja juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika muda na saa ambao tutapanga kwa pamoja na Wizara tupo tayari kukutana na UWAWAME ili twende tukaone namna gani ya kuwaongezea tija katika uzalishaji wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.
Name
Yannick Ikayo Ndoinyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ngorongoro
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 5
MHE. YANNICK I. NDOINYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Langu ni ombi na ushauri kwa Wizara kufanya utafiti wa uzalishaji wa zao la maziwa katika Wilaya yangu ya Ngorongoro ili kuwashauri na kuwasaidia wazalishaji wa maziwa wapate soko la uhakika na kuongeza kipato chao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ushauri na ombi kwa Wizara. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru sana, ninamshukuru sana Mbunge wa Ngorongoro, ushauri wake ni mzuri na tumeupokea kwa ajili ya kuufanyia kazi. Ahsante sana.
Name
Charles Jacob Sungura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Vijijini
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Supplementary Question 6
MHE. DKT. CHARLES J. SUNGURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nipate majibu kwa Naibu Waziri kwamba, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kituo cha kukusanyia maziwa kilichopo katika Kijiji cha Msomela, Kata ya Misima?
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti ninakushukuru sana. Kadri ya upatikanaji wa fedha ndivyo ambavyo Serikali itaendelea na ujenzi wa kituo hiki cha ukusanyaji wa maziwa kilichopo Msomela. Nakushukuru sana.