Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 7 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 63 | 2026-04-13 |
Name
Timotheo Paul Mnzava
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Vijijini
Primary Question
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa?
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Ninaomba sasa nijibu swali la Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini, kama Ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Taasisi ya Bodi ya Maziwa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Chama cha Ushirika cha Wazalishaji Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU), wanaendelea na utatuzi wa changamoto za kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga almaarufu kama Tanga Fresh ambacho kina uwezo wa kusindika maziwa lita 120,000 kwa siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kiwanda hicho ndicho soko kubwa la maziwa yote ya Mkoa wa Tanga na Mikoa ya jirani. Changamoto za kiwanda hicho ni pamoja na upungufu wa mtaji na gharama kubwa za uendeshaji na hivyo kushindwa kununua maziwa ya wafugaji kwa bei ya uhakika. Kutatuliwa kwa changamoto hizo kutasaidia wafugaji wa Korogwe vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatekeleza mradi wa miaka kumi wa mageuzi ya tasnia ya maziwa na mabadiliko ya tabianchi katika Mikoa 13 nchini, Mikoa nane Tanzania Bara na Mikoa mitano Zanzibar ikiwemo Mkoa wa Tanga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo utaboresha mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo vituo vya kukusanyia maziwa kutoka kwa wafugaji kabla ya kupeleka kiwandani. Hatua hizi, zitasaidia wafugaji wa Korogwe Vijijini na Mkoa wa Tanga kwa ujumla kupata soko na bei ya uhakika ya maziwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved