Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Salum Motto

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA S. MOTTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri ya kutia moyo wananchi wa Mkoa wa Mtwara. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, tayari kuna mwekezaji huyu Soil Solution, ambaye kimsingi kwa taarifa za awali mwekezaji huyu tayari ameshalipa fidia wananchi wa Mgau, kwa maana ya Halmashauri ya Mtwara DC, ekari 151 za ardhi kwa shilingi 1,832,000,000; kwa taarifa rasmi, kiwanda hiki kikikamilika kinatarajia kuajiri wafanyakazi 3,000, lakini pia, kinatarajia kugharimu uwekezaji wa Dola za Kimarekani 627,000,000. ni nini Kauli ya Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda hiki mpaka sasa hakijaanza kufanya kazi. Wananchi wa Mkoa wa Mtwara, kwa maana ya Mtwara DC, walikuwa na matumaini makubwa sana baada ya kuona kuwa wamelipwa fidia, wakijua kabisa utekelezaji unaenda kuanza kufanya kazi kwa muda siyo mrefu na mwekezaji huyu yupo nchini hapa Tanzania mwaka mmoja sasa…

MWENYEKITI: Umeeleweka Mheshimiwa Asha. Uliza swali la pili, kama unalo.

MHE. ASHA S. MOTTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Kwa kuwa, Mikoa ya Kusini ina rasilimali ya gesi na makaa ya mawe, na tayari tumeona kuna wawekezaji wamewekeza katika rasilimali hii ya gesi; ni nini Kauli ya Serikali juu ya uwekezaji wa makaa ya mawe? Maana tuna bandari tayari inayosafirisha makaa ya mawe, pia Mkoa wa Mtwara tuna njia kuu ya kupitisha hayo makaa ya mawe. Ninaomba kujua Serikali ina mkakati gani kukaribisha wawekezaji wanaotumia makaa ya mawe? Ahsante.

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Asha Salum Motto, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Mtwara, kwa jinsi anavyowatetea wananchi. Mheshimiwa Asha amenisumbua sana kuhusu huyu mwekezaji ambaye anaitwa Soil Solution, ambaye kimsingi ni kweli ameshanunua zaidi ya ekari 150 na amelipa fidia zaidi ya shilingi bilioni 1.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yetu pamoja na Wizara ya Nishati tumekuwa tukifanya majadiliano kuona ni jinsi gani tunaweza tukamsaidia mwekezaji huyu ili aanze ujenzi wa kile kiwanda chake? Majadiliano yanaenda vizuri. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, sisi kama Serikali, tunafanyia kazi na tupo hatua nzuri ya kuhakikisha mahitaji yote ya mwekezaji yanafanyiwa kazi na tunaona tija ya uwekezaji huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwekezaji huyu anakuja kutengeneza ajira zaidi ya 3,000, na anakuja kuwekeza zaidi ya Dola za Kimarekani zaidi ya milioni 627 Mkoani Mtwara. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, sisi kama Serikali, tupo. On top of that tutahakikisha tunamsaidia na tunawasaidia wawekezaji wote wanaokuja nchini, ili wawe na mazingira rafiki, kwa ajili ya uwekezaji wao kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni kweli, sisi kama Serikali na Tanzania, tuna makaa ya mawe ya kutosha na Mtwara ni lango la kupitisha makaa ya mawe. Tunapofanya uhamasishaji wa wawekezaji, mojawapo ya eneo ambalo tunalihamasisha ni jinsi gani wawekezaji wanaweza kuja Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuwekeza wakitumia nishati ya makaa ya mawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba, tutachukua suala la Mkoa wa Mtwara kama kipaumbele tunapozunguka huko duniani na hapa Tanzania kuwahamasisha wawekezaji waje kuwekeza Mtwara. Nashukuru.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ninakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Guta, kwenye Jimbo la Bunda Mjini, kuna eneo la Tairo ambalo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji na wananchi wameshalipwa fidia. Eneo hili limekaa wazi zaidi ya miaka 14. Naibu Waziri ameenda kulitembelea eneo lile, eneo ambalo ni very potential, liko karibia na Ziwa na lipo kwenye lami. Je, ni lini sasa wataletwa wawekezaji, wajenge viwanda ili akina mama wa Bunda na Vijana wa Bunda waweze kupata ajira? (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Bulaya, amekuwa akinisumbua sana kuhusu ile Bunda SEZ, ambayo kimsingi ni mojawapo ya vipaumbele vya Serikali. Kama tunavyotambua, Rais amesisitiza kwamba tunaenda kuanzisha kongani za viwanda, lakini mojawapo ya mkakati wetu sasa hivi tunaenda ku-promote uwekezaji kwenye maeneo ya SEZ. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunda ni mojawapo ya meneo ambayo kimsingi ni mkakati wa Serikali na katika bajeti yetu ya mwaka huu imo, na tunaenda kutenga eneo kwa ajili ya uwekezaji wa vijana. Ninaomba nimhakikishe Mbunge kwamba suala la Bunda SEZ tumelipa kipaumbele. Ahsante.

Name

Arif Suleiman Premji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Supplementary Question 3

MHE. ARIF S. PREMJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji wa Soil Solution ni wa kimkakati, unaenda kusaidia Taifa hili kupunguza gharama ya Dola za Kimarekani milioni 400 kwa kuagiza mbolea. Majibu ambayo yametolewa ni mepesi mno, uhitaji wa Soil Solution ni gesi na gesi inatoka Mtwara, hadi sasa hivi ni mwaka mzima anazungushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipi kauli rasmi ya Serikali kuhusiana na mradi huo wa kimkakati ambao unaenda kusaidia Taifa letu? (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mbunge kutoka Mtwara, Ndugu yangu, Mheshimiwa Arif, amekuwa akiniuliza sana swali hili, amekuwa akifuatilia sana kuhusu huyu mwekezaji ambaye kimsingi anatoka Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba Soil Solution Limited ni mojawapo ya uwekezaji wa kimkakati, kulingana na vigezo vyetu, mwekezaji yeyote wa nje anapokuja kuwekeza akiwa na zaidi ya milioni 50 USD ni mwekezaji wa kimkakati, huyo wa kwetu ana zaidi ya milioni 150, anazo milioni 627 za Kimarekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotangulia kujibu kwenye swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha Motto, naomba niseme kwamba Serikali ipo on top of that, na tumekuwa na majadiliano na wenzetu wa Wizara ya Nishati. Ninamshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Ndejembi, amekutana mara nyingi sana na huyu mwekezaji na wamemhakikishia kwamba baada ya mipango ya upatikanaji wa gesi itakapokuwa vizuri, tunamhakikishia ujenzi wa kiwanda utaanza. Nashukuru. (Makofi)

Name

Zuberi Yahya Mfaume

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Supplementary Question 4

MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Morogoro Vijijini kwa sasa ndiyo mzalishaji mkubwa wa karafuu. Wawekezaji kutoka Indonesia walionesha nia ya kutaka kuwekeza katika eneo letu. Je, Wizara ina mpango gani sasa wa kuendelea kuvutia wawekezaji ili wakaweke viwanda vya kusindika karafuu kule Morogoro DC? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mbunge kwa swali lake zuri la kutetea watu wa Morogoro, hususan kwenye suala la kilimo cha karafuu na haja ya kupeleka viwanda na wawekezaji Morogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, kipaumebele chetu ni kuvutia wawekezaji. Rais ameshatuagiza, lakini ninyi wenyewe ni mashahidi Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa kipaumbele katika kuvutia wawekezaji anapozunguka huko duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue suala la Morogoro kama kipaumbele, nasi tutaliweka kwenye mpango wetu wa kuhamasisha na kuvutia wawekezaji waje kuwekeza Morogoro. Ninashukuru.

Name

Morris Joseph Makoi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Supplementary Question 5

MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Ninaomba niulize kwamba hapa Dodoma kuna kiwanda cha mbolea, na hivi karibuni na hapa ninapoongea katika Jimbo la Moshi Vijijini wananchi wanataabika sana kutafuta mbolea ya ruzuku na mbolea mpaka sasa haipatikani kwa ajili ya palizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inatuambiaje kuhusiana na uzalishaji wa kiwanda cha mbolea hapa Dodoma na kama mbolea ile inaweza ikapelekwa katika Mikoa hususan Kilimanjaro na Jimbo la Moshi Vijijini ili kusaidia kupunguza taabu ya mbolea katika Jimbo lile wakati huu wa palizi? (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mbunge kutoka Moshi Vijijini kwa swali lake zuri la kuwatetea Wananchi wa Moshi ambao ni wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana kwamba tunacho kiwanda kikubwa cha ITRACOM cha hapa Dodoma ambacho kipo maeneo ya Nala. Ni mwekezaji mkubwa wa kimkakati ambaye kimsingi amesaidia sana kupunguza tatizo la mbolea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakiri kwamba bado tuna changamoto katika suala la mbolea na ndiyo maana Serikali tumeweka mkazo kuvutia wawekezaji wa viwanda vya mbolea. Kwa hiyo, ninaomba Mbunge akubaliane nasi kwamba, wakati Serikali inajipanga kuvutia wawekezaji, tutaendelea kutumia viwanda vilivyopo kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa ajili ya kilimo. Ninashukuru.