Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 7 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 62 2026-04-13

Name

Asha Salum Motto

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA S. MOTTO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kukaribisha wawekezaji wa viwanda vya mbolea na saruji, Mtwara, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe?

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Asha Salum Motto, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mtwara, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na uwepo wa makaa ya mawe na rasilimali ya gesi asilia katika Mikoa ya Kusini, ukiwemo Mkoa wa Mtwara, kampuni kadhaa za uwekezaji zimevutiwa kuwekeza katika mikoa hiyo. Miongoni mwa kampuni kubwa za uwekezaji za nje zilizowekeza Mtwara baada ya kuvutiwa na mazingira hayo ni pamoja na Kampuni ya Dangote Cement kutoka Nchini Nigeria, ambayo imewekeza katika kiwanda cha saruji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Kampuni ya Indorama ya Nigeria na Soil Solution ya India zimeonesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya mbolea, ambapo Kampuni ya Soil Solution imeanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea ndani ya eneo lililopo Mtwara Mjini. Ofisi inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya mbolea na saruji kupitia mikutano na makongamano ya wawekezaji yanayofanyika ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.