Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka Mradi wa Majisafi Kata ya Mpinji kwa Vijiji vyote vinne?
Supplementary Question 1
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, Kata hii ya Mpinji ina wananchi takribani 10,999, kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022. Ukizunguka vijiji vyote vinne hutakutana na bomba la maji salama hata moja. Je, Serikali haioni kwamba wananchi hawa 10,999 wanaishi maisha hatarishi, wakalichukua suala hili la maji Kata ya Mpinji kwamba ni suala la dharura sana?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana, na nimshukuru sana Mheshimiwa Anne Kilango Malecela. Kwanza kabisa nampongeza, wakati anaingia katika Jimbo la Same Mashariki, huduma ya maji ilikuwa mbaya sana. Mpaka sasa tunapoongelea kati ya vijiji vile 1,575, na vijiji vyake ambavyo ni vinne lakini kuna kata nyingine pia ambapo ndiyo wamebaki kuwa wana changamoto ya maji.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunalichukua kwa uzito stahiki ili eneo hili kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Mpinji waweze kupata huduma ya majisafi na salama kulingana na mahitaji ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyasema.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuwekeza vizuri kuhakikisha vijiji vyote 1,575 vinapata huduma ya majisafi na salama ili kukamilisha vijiji 12,333 nchi nzima ambavyo wananchi ndiyo wanaishi katika maeneo hayo na wanahitaji upatikanaji wa majisafi na salama.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka Mradi wa Majisafi Kata ya Mpinji kwa Vijiji vyote vinne?
Supplementary Question 2
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, haya, sawa Mheshimiwa Mbunge wa Ilala. Ninakushukuru kwa nafasi. Naomba kujua, mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria una gharama ya shilingi bilioni 134, ni mkubwa; na nimeomba mara kadhaa kwenye Bunge hili kwamba matoleo ya tenki la maji Sirari, Mogabiri na Komaswa yawekwe.
Mheshimiwa Spika, sasa naomba kama Serikali ipo tayari kunipa majibu kwa maandishi kuhusu commitment hiyo, kwa sababu maelezo ambayo waliniambia kule Tarime ni tofauti kabisa na maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri wamenijibu huku Bungeni. Je, wanaweza wakanipa hayo majibu ya maeneo hayo matatu matoleo ya mradi ule kwenye jimbo langu kwa maandishi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa swali hili kwanza alishaliuliza Mheshimiwa Waitara na alishatoa ushauri na Seriklai tulipokea ushauri na tulituma wataalam wetu walikwenda kufanyia kazi kulingana na yale matoleo ambapo alikuwa anahitaji ishuke kwa wananchi ambao walikuwa wanayahitaji.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Serikali inaendelea kulifanyia kazi. Hivyo, nimwombe awe na subira kidogo ili Serikali ihakikishe kwamba utaalam umezingatiwa katika kuhakikisha kwamba maji yanapokwenda kutolewa kwa ajili ya vile vijiji, basi kusiwe na madhara yoyote.
Mheshimiwa Spika, pia Serikali iko tayari kutoa commitment kwa maandishi ili kuhakikisha kwamba wananchi wake wa Jimbo la Tarime wawe na uhakika wa upatikanaji wa maji kutokana na miundombinu ambayo tayari imeshajengwa. Ahsante sana.
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka Mradi wa Majisafi Kata ya Mpinji kwa Vijiji vyote vinne?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini wananchi wa Kata ya Ng’ang’ange mkandarasi atapatiwa fedha ili ule mradi uweze kukamilika kwa sababu ule mradi umesubiriwa kwa muda mrefu sana na pale hakuna kisima chochote, wananchi wanapata mateso hakuna majisafi na salama?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mradi huu bahati nzuri ninaufahamu na nilifika pale kwa ajili ya uzinduzi wake. Nimhakikishie katika Mradi huu wa Ng’ang’ange, mkandarasi tayari yuko site na tayari anaufanyia kazi na tuko kwenye ujenzi wa tenki. Kikubwa tu ni kwamba tunafahamu mkandarasi alikuwa amewasilisha hati za madai, na tayari Serikali inafanyia kazi hati yake ya madai yaweze kulipwa na kuharakisha ukamilishaji wa mradi huu ili wananchi wa Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati wapate huduma ya maji safi na salama. Ninakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved