Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 2 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 9 | 2026-04-01 |
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: -
Je, Serikali haioni umuhimu wa kupeleka Mradi wa Majisafi Kata ya Mpinji kwa Vijiji vyote vinne?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba vijiji vyote 12,333 vilivyopo nchini vinafikiwa na huduma ya majisafi na salama kufikia mwaka 2030. Aidha, hadi sasa jumla ya vijiji 10,758 vimeshafikishiwa huduma ya majisafi na salama kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji katika vijiji 1,575 vilivyobaki, ikiwemo vijiji vinne vya Mpinji, Sambweni, Kirongwe na Ivuga vilivyopo Kata ya Mpinji Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved