Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: - Je, tangu kurejeshwa kwa Export Levy kwenda Bodi ya Korosho Tanzania ni kiasi gani kimekusanywa hadi sasa na kimetumikaje?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ninaomba niseme kwamba majibu yaliyojibiwa yamekuwa too general, na hizi fedha ni za wakulima, bila shaka wangetamani kufahamu kinagaubaga jinsi fedha zao zinavyotumika baada ya kukatwa.
Mheshimiwa Spika, sasa kuna majibu ya kusema kwamba wamepewa wazabuni, wamelipiwa wazabuni, lakini wazabuni hao ni wapi? Halikadhalika, zimelipwa kwa ajili ya maendeleo. Je, miradi hii ya maendeleo ni ipi, kwa sababu swali linaonekana limeulizwa vizuri, lakini majibu yamefungwafungwa. Bado tunahitaji kufahamu, ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nimshukuru Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Lulindi kwa maswali yake ya msingi. Sisi kama Wizara kupitia Bodi ya Korosho tuko tayari kumpatia orodha ya wazabuni wote waliolipwa pamoja na miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia fedha hizi za Export Levy ambazo Bodi imepokea. Kwa hiyo, kwa sababu ni orodha kubwa, tutampatia.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved