Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 7 2026-04-01

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: -

Je, tangu kurejeshwa kwa Export Levy kwenda Bodi ya Korosho Tanzania ni kiasi gani kimekusanywa hadi sasa na kimetumikaje?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Lulindi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2024/2025 hadi Februari, 2026 Bodi ya Korosho Tanzania imepokea fedha za Export Levy jumla ya shilingi bilioni 350.63. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 183.58 zilipokelewa mwaka wa fedha 2024/2025 na shilingi bilioni 167.06 zimepokelewa mwaka 2025/2026 kufikia Februari, 2026.

Mheshimiwa Spika, kati ya jumla ya fedha hizo zilizopokelewa, ni kiasi cha shilingi bilioni 339.17 kimetumika kulipa madeni ya wazabuni wa pembejeo za korosho zilizotolewa kwa wakulima kwa ruzuku ya 100%, na shilingi bilioni 11.46 zimetumika kugharamia miradi ya maendeleo katika tasnia ya korosho.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania itaendelea kulipa madai ya wazabuni na kulipia gharama za pembejeo kwa wakulima.