Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Primary Question

MHE. NAPE M. NNAUYE aliuliza: - Je, Serikali ipo tayari kupitia upya mfumo wa bei kwenye minada ya korosho kwa kuwa kuna malalamiko ya namna bei zinavyopatikana?

Supplementary Question 1

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa kwa mfumo tulionao sasa hivi, katika msimu mmoja wa korosho kuna uwezekano wa bei ikapishana sana, wakati mwingine kutoka shilingi 4,000 kwenda mpaka shilingi 2,000. Hili gap ni kubwa sana katika msimu mmoja wa uuzaji wa korosho.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali iko tayari kushirikiana na wadau kwenda kupitia upya mfumo huu ili kupunguza gap hili tuwape wakulima wetu faida wanayostahili kuipata?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwenye maghala haya ambayo yanahifadhi korosho, katika wakati mmoja ghala moja linachukua korosho za wakulima wengi; na wakati tunakwenda mnadani, wanaokuja kununua wakati mwingine wanakuja wananunua korosho kidogo kidogo na kwa bei tofauti tofauti, jambo ambalo linapelekea sintofahamu korosho ya nani inakwenda kwa bei gani, kutoka kwenye ghala moja la wauzaji wa korosho.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali iko tayari tuupitie upya mfumo huu ili tuwatendee haki wakulima kwa kuongeza uwazi, na kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanatendewa haki kwenye bei na uuzaji wa korosho yao?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninamshukuru Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Mbunge wa Mtama kwa maswali ya msingi hususan kwenye tasnia ya korosho.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la kwanza, jambo moja ambalo ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, sisi kama Serikali tupo tayari kushirikiana na wadau kukutana pamoja na kuhakikisha kwamba tunaangalia huu mfumo kutoka eneo moja mpaka lingine ili kuhakikisha kwamba mfumo huu unanufaisha wakulima.

Mheshimiwa Spika, kuhusu tofauti ya bei hususan katika maeneo ya maghala, na lenyewe namthibitishia tu Mheshimiwa Mbunge, hatutakubali kwenda katika mfumo ujao bila kukaa pamoja na wadau na kupitia upya ili kuhakikisha wakulima ndio wanakuwa wanufaika wakubwa. Kwa hiyo, ninamthibitishia tu, kwamba Serikali tuko tayari na tutalifanya hivyo.