Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 2 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 6 | 2026-04-01 |
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Primary Question
MHE. NAPE M. NNAUYE aliuliza: -
Je, Serikali ipo tayari kupitia upya mfumo wa bei kwenye minada ya korosho kwa kuwa kuna malalamiko ya namna bei zinavyopatikana?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, ninaomba kujibu Swali la Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Mbunge wa Mtama, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Korosho Tanzania imeendelea kushirikiana na wadau kuendesha minada kwa njia ya kidijiti kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kwa lengo la kuongeza uwazi, ushindani na kuimarisha bei ya mkulima. Hatua hiyo imesaidia uwazi na upatikanaji wa bei shindani kwa wakulima kulingana na upatikanaji na mahitaji ya korosho kwa wakati husika.
Mheshimiwa Spika, katika msimu wa 2025/2026, korosho za Tanzania ziliuzwa kwa wastani wa shilingi 2,550 kwa kilo, ikilinganishwa na wastani wa shilingi 1,750 kwa kilo katika nchi za Msumbiji, Ivory Coast, Ghana, Nigeria na Benin. Hali hiyo inadhihirisha kuwa Mfumo wa TMX una mchango mkubwa katika upatikanaji wa bei shindani kwa wakulima kulingana na hali ya Soko la Dunia.
Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri ili kufanya maboresho zaidi pale inapobidi ili kuendelea kuimarisha mfumo wa uuzaji wa korosho kwa manufaa ya wakulima.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved