Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Enock Zadock Koola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. ENOCK Z. KOOLA aliuliza :- Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha chakula katika Jimbo ya Vunjo?
Supplementary Question 1
MHE. ENOCK Z. KOOLA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Mheshimiwa Rais kwenye sekta ya kilimo, ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa Serikali ilitangaza mpango wa kuchimba visima virefu 500 nchi nzima kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Je, Serikali inaweza kutoa taarifa kuhusu idadi ya visima vilivyopangwa kutekelezwa katika Jimbo la Vunjo ili kusaidia vijana na wanawake wanaoshughulika na kilimo cha mbogamboga?
Mheshimiwa Spika, pili, kwa kuwa tayari Serikali imeanza kutekeleza ahadi ya kutoa miche mipya ya kahawa na tulishazindua hiyo ziara kwenye Jimbo letu la Vunjo kwa wakulima wa Jimbo la Vunjo, je, Serikali ina mkakati gani wa kufufua skimu ya mifereji ya asili, ukanda wa juu itakayowawezesha wakulima kumwagilia miche hii mipya ya kahawa? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nami ninampongeza Mheshimiwa Koola, Mbunge wa Vunjo kwa maswali yake ya msingi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha ambao tunaendeleanao, na katika bajeti ya kilimo tulikuwa tumepanga kuchimba walau visima vitano katika kila Jimbo nchini kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji.
Mheshimiwa Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Wizara ya Kilimo tumesha-hire magari kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji pamoja na Wizara, kupitia miradi mbalimbali tuliyonayo pale, wanaendelea na shughuli hiyo.
Mheshimiwa Spika, namhakikishia tu kwamba tayari Wizara ya Kilimo tumeshapokea magari kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo. Tume ya Taifa ya Umwagiliaji pamoja na Wizara kupitia miradi mbalimbali tuliyonayo pale, wanaendelea na shughuli hiyo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kufufua skimu za asili kwa ajili ya kumwagilia kahawa, hilo ndilo jukumu letu. Tunaendelea kuzifufua zile za asili pamoja na kuzikarabati zilizopo ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Vunjo na maeneo mengine nchini wananufaika na Wizara ya Kilimo ambayo ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais. Ahsante sana.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. ENOCK Z. KOOLA aliuliza :- Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha chakula katika Jimbo ya Vunjo?
Supplementary Question 2
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali ilifanya feasibility study ya skimu kubwa za Wilaya ya Hai Metrom, Bolutu, Makeresho, Kikafu Chini na Longoi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa skimu hizi pamoja na zile skimu ndogo, kwa maana ya mifereji?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge wa Hai Comrade Saashisha, kwamba tukishamaliza hatua ya usanifu, ambapo katika baadhi ya maeneo ambayo ameyataja hapa yakiwemo Mbokomu pamoja na Makeresho, tumeshakamilisha. Hatua inayofuata sasa hivi ni kutangaza kwa ajili ya kupata mkandarasi, na baada ya hapo mkandarasi akabidhiwe site na kuanza kazi ya ujenzi wa mabwawa pamoja na skimu katika maeneo hayo.
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENOCK Z. KOOLA aliuliza :- Je, lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha chakula katika Jimbo ya Vunjo?
Supplementary Question 3
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa Serikali iliwaahidi wakulima wadogo wadogo wa kilimo cha miwa katika eneo la Bagamoyo kwa ajili ya Kiwanda cha Sukari cha Bakhresa, na kwa kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa maji, je, Serikali ule mpango wake wa ujenzi wa bwawa la umwagiliaji kwa ajili ya kuwasaidia wakulima hawa na kiwanda cha sukari Bagamoyo unaendeleje?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Niungane na Mheshimiwa Mbunge wa Bagamoyo, Mheshimiwa Subira Mgalu kumhakikishia tu kwamba mpango wa Serikali unaendelea, na tupo katika hatua za mwisho za usanifu wa mradi ule. Mara baada ya kukamilika, tutaingia katika hatua inayofuata ya kutangaza na kupata mkandarasi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa maeneo hayo.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved