Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: - Je, lini ahadi ya kuwapatia maeneo wakazi wa Kata za Lukozi, Shume na Manolo kutoka Shamba la miti Shume itatekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninashukuru kwa majibu mazuri sana ya Serikali kwamba wameridhia kutoa eneo hili kwa ajili ya shughuli za kijamii kama ambavyo amesema. Kwa hiyo, ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa usikivu wake kwa sababu alivyokuja Februari mwaka 2025 tulimpa hili ombi na sasa Wizara imeridhia kugawa eneo hili. Nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, huu ni utekelezaji wa ahadi ya Rais ambayo ameitoa kwa wananchi wa Lushoto, ni kwa haraka kiasi gani maeneo haya yaliyoombwa kumegewa maeneo kutoka Shamba la Miti Shume utekelezaji utaanza?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninamshukuru Mbunge wa Mlalo, Mheshimiwa Rashid Shangazi na tumepokea shukrani kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, na kwa sababu haya ni maelekezo yake na hatua karibu zote tumeshazifanya.

Mheshimiwa Spika, ninakuthibitishia, kuanzia mwaka wa fedha unaoanza, Serikali itakuwa tayari kutoa maeneo hayo kwa ajili ya wananchi. Ahsante sana.