Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 2 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 4 | 2026-04-01 |
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -
Je, lini ahadi ya kuwapatia maeneo wakazi wa Kata za Lukozi, Shume na Manolo kutoka Shamba la miti Shume itatekelezwa?
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua ahadi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuangalia uwezekano wa kupata ardhi kidogo kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii kama ilivyoombwa na Mheshimiwa Mbunge wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Wilayani Lushoto mwezi Februari, 2025.
Mheshimiwa Spika, Wizara ilianza kufanyia kazi maelekezo hayo kwa kufanya uchambuzi wa maombi mbalimbali yaliyowasilishwa na ofisi mbalimbali kuanzia ngazi za Vijiji, Kata na Halmashauri ya Lushoto yakiomba kumegewa maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.
Mheshimiwa Spika, baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa, Wizara iko tayari kumega sehemu ya eneo la shamba hilo kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa shule na eneo la maziko.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved