Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga daraja litakalounganisha Tarafa ya Mkongo kati ya Kata ya Mkongo na Utete ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji?
Supplementary Question 1
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, na pia namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mpango wa ujenzi wa Daraja la Mto Utete ni mpango wa muda mrefu, lakini pia ni mpango wenye gharama kubwa; na kwa kuwa Barabara ya Ikwiriri hadi Mkongo tayari ilishapembuliwa na ilishasanifiwa, imebakia tu hatua ya Wizara ku-sign ili ujenzi wa lami uanze. Swali langu, ni lini Wizara ita-sign mkataba huu ili ujenzi wa lami uanze?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Kivuko kilichopo Mto Utete ni kidogo. Je, Serikali itakuwa tayari kutupatia kivuko kikubwa kitakachoweza kusaidia wananchi wa kata hizi mbili na tarafa moja? Ahsante.
Name
Eng. Edwin Amandus Ngonyani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tayari tulishasanifu barabara ya kutoka Ikwiriri hadi Mkongo na kinachosubiriwa ni kibali cha barabara hiyo iweze kutangazwa ili ianze kujengwa kwa lami. Kwa sasa barabara hiyo ipo kwa kiwango cha changarawe na bahati nzuri katika barabara hiyo pia kuna daraja kubwa la Mbambe ambalo mkandarasi yupo site, anajenga daraja hilo pamoja na kilomita tatu kwa kiwango cha lami ambayo sasa itaunganisha Ikwiriri na Mkongo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunapokea kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge kwamba tuharakishe kusaini ama kutangaza hiyo barabara ili ianze kujengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusu kivuko, kivuko kipo na kimefanyiwa ukarabati. Kwa hiyo, tutafanya tathmini kupitia TEMESA, kuona mahitaji ili kama kuna umuhimu wa kuongeza uwezo wa kivuko, basi kiweze kujengwa kipya kati ya Mkongo na Utete, ahsante.
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga daraja litakalounganisha Tarafa ya Mkongo kati ya Kata ya Mkongo na Utete ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji?
Supplementary Question 2
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nilitaka kufahamu, Serikali imefikia hatua gani katika ujenzi wa barabara ya kutoka Mlowo kwenda Kamsamba? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Mlowo kwenda Kamsamba, Serikali ilishaahidi kujenga kilomita 10; na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka huu ambao tayari ilishatangazwa na ilishapata mkandarasi, kwa hiyo, sasa hivi Serikali inatafuta fedha advance, yaani kwa maana ya malipo ya awali ili mkandarasi ambaye amepatikana kuanza kazi hiyo ya kujenga kilomita 10, ahsante.
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga daraja litakalounganisha Tarafa ya Mkongo kati ya Kata ya Mkongo na Utete ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji?
Supplementary Question 3
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuuliza swali kwenda Wizara ya Ujenzi kwamba, ni lini daraja linalounganisha Kata ya Tawa na Kata ya Konde vitakwenda kutengenezwa kwa maana limeshavunjika na hakuna mawasiliano katika kata hizo mbili? Ahsante.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwa ufupi.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, sijamsikia vizuri Mheshimiwa Mbunge, hilo daraja na…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge taja daraja hilo kwa sauti usikike.
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Naibu Spika, daraja hilo ni Daraja la Mto Mfizigo ambalo linaunganisha Kata ya Tawa na Kata ya Konde, kwa sasa hakuna mawasiliano baina ya kata hizi mbili na hii ni Barabara ya Kiswila kuelekea Tawa, ahsante.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, labda ungetaja na jimbo maana kata na kata pengine kwa Mheshimiwa Waziri inaweza ikawa ngumu.
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, katika Jimbo la Morogoro Kusini Barabara ya Msalabani kwenda Tawa katikati kuna Daraja la Mto Mfizigo ambalo linaunganisha Kata ya Tawa na Kata na Konde, daraja hili sasa hivi halipitiki kabisa.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nimpe pole Mheshimiwa Mbunge, lakini pia na wananchi ambao wamekumbwa na adha hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe tu maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Morogoro kwa sababu ni kweli katika kipindi cha mvua madaraja mengi yamekatika na yanashindwa kupitika, lakini pia hata maeneo mengine ambayo barabara zimekatika.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunachofanya labda tu kwa ujumla ni kwamba tumeshatoa maelekezo kwa mameneja wote wa mikoa, kufanya tathmini na kila siku kuleta taarifa Makao Makuu ya TANROADS na Wizara ili Serikali wakati inatafuta hizi fedha za dharura, basi ziweze kwenda kurudisha mawasiliano kwa dharura tukiwa tunajipanga kufanya matengenezo ama ujenzi wa kudumu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitoe maelekezo specifically kwa Meneja wa Mkoa wa Morogoro ahakikishe anafika eneo hilo, achukue hatua za haraka kwanza kurejesha mawasiliano ya muda wakati Serikali inatafuta fedha kulijenga hilo daraja kwa upya, ahsante.
Name
Kijakazi Mohamed Yunus
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga daraja litakalounganisha Tarafa ya Mkongo kati ya Kata ya Mkongo na Utete ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji?
Supplementary Question 4
MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Naomba kufahamu wananchi wa Kata ya Nanjirinji Wilayani Kilwa Mkoani Lindi wamekuwa wakipata adha ya kuvuka Mto Mbwemkuru kuelekea Wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya kufuata huduma za dharura. Daraja hili lilisombwa na masika mwaka 2024. Sasa nataka kufahamu, je, ni lini Serikali itajenga daraja hili ili kuwaondolea wananchi hawa adha hususan wanawake wajawazito?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge, na bahati nzuri hilo daraja nilipita kabla na hata baada ya kusombwa. Ni barabara ambayo inaunganisha Ruagwa – Nanjirinji hadi Kiranjeranje.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ule mpango wa kujenga madaraja ya dharura, kulikuwa na madaraja matatu katika hiyo barabara. Moja, ni hilo Mbwemkuru ambayo ni daraja kubwa, mto mkubwa, na pia tuna Daraja Nakiu na Kigombo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Nakiu na Kigombo yamekamilika. Hili daraja la Mbwemkuru liko kwenye mpango wa kujengwa na mfadhili wa World Bank kwenye kuratibu mradi unaoitwa CRW; inavyosema, mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kuanza kulijenga hilo daraja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni taratibu tu, zikikamilika na wenzetu wa World Bank, daraja hilo linaweza kujengwa ili kuondoa hiyo adha, ahsante.