Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 3 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 19 | 2026-04-02 |
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga daraja litakalounganisha Tarafa ya Mkongo kati ya Kata ya Mkongo na Utete ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa daraja unahusisha hatua mbalimbali ikiwemo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya usanifu wa daraja linalounganisha Kata ya Mkongo na Utete. Kazi hiyo itakapokuwa imekamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved