Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwa sera yake ya kuhakikisha kuwa maji ya Ziwa Victoria yanakwenda kwenye mikoa au miji iliyolizunguka, hususan Muleba. Swali dogo la nyongeza, Mheshimiwa Naibu Waziri anakumbuka ombi letu la Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria pale Kasharunga kwenda Muleba Magharibi? Je, ni lini upembuzi na usanifu wa kina kwa ajili ya kutoa maji Kasharunga - Mubunda - Nyakatanga - Mushabago, kwenda Ngenge na Rutoro utaanza?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge ambaye anaendelea kushirikiana vizuri sana na wananchi wake kutatua changamoto za maji kwa kuwasemea katika Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ambao ni wa kimkakati ambao Mheshimiwa Mbunge amekuwa akiusemea mara kwa mara na sisi Serikali tumeona ni vyema sasa tukauingiza katika hatua za utekelezaji. Nimtoe hofu kwamba mwaka wa fedha 2025/2026 mradi huo utaanza kufanyiwa upembuzi yakinifu katika hatua za awali za na baadaye tutafanya detail design kwa ajili ya kujua kwamba sasa gharama gani zitahitajika kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mradi huo unatekelezwa. Ahsante sana.
Name
Christopher Olonyokie Ole-Sendeka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Simanjiro
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 2
MHE. CHRISTOPHER O. OLE – SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa Wizara imeshatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kwamba maji safi na salama ya mradi wa shilingi bilioni 500 wa Arusha unapelekwa Kata za Mererani na Endiamtu, kwa sasa bado Kata ya Shambarai, Naisinya na Oljoro namba tano ambapo Mheshimiwa Rais alielekeza maji yale yafike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa Serikali itatekeleza mradi huo ikiwa ni pamoja na Kata ya Msitu wa Tembo ambayo madini ya flouride yanaharibu meno ya watu na pia kupindisha watoto miguu?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Ole-Sendeka na kwa kutambua uwekezaji mkubwa sana uliofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuwekeza shilingi bilioni 500, pia, ninafahamu kabisa kwamba kuna maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuendelea kutekeleza mradi katika maeneo ya Mererani, Msitu wa Tembo na pia utekelezaji upo chini ya Wizara ya Maji tu umeshaanza na utekelezaji huu unaenda hatua kwa hatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu, maeneo yote ambayo Mheshimiwa Rais ameshaelekeza na maeneo mengine ambayo ni mpango wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi, tutahakikisha kwamba tunawapelekea huduma ya maji ili waweze kuondokana na madini ya flouride ambayo yamekuwa yakiwatesa sana wananchi wa maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 3
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Pamoja na kuishukuru Serikali kwa kazi kubwa inayoendelea ya kutoa maji kutoka Lake Victoria kwenda Urambo, je, ni lini sasa Serikali itaanza kuweka miundombinu ya maji itakayowezesha kufikisha maji katika tanki litakalokusanya maji hadi kuwafikia wananchi kutokana na shida kubwa ya maji tuliyonayo? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana mama yangu Margaret Simwanza Sitta kwa kazi kubwa ambayo ameendelea kuifanya kwa wananchi wake wa Urambo. Tunatambua kabisa kwamba Serikali iliwekeza zaidi ya shilingi bilioni 680 kuyatoa maji kutoka ziwa victoria mpaka Tabora, lakini pia Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 143 kwa ajili ya Kaliua, Urambo pamoja na Sikonge. Tunatambua kwamba mradi huu umefikia asilimia nzuri sana za utekelezaji zaidi ya 70%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba mradi huu wakati unatekelezwa, pia kulikuwa na mtandao wa zamani ambao ulikuwa unawahudumia wananchi wa Urambo. Sasa kazi ambayo tunaifanya kwa sasa, kwa sababu tanki limeshakamilika, ni kuanza kupeleka maji kwenye mtandao wa zamani, wakati mradi ukiwa unaendelea wa kuondoa mtandao wa zamani na kuweka mtandao mpya, lakini wananchi waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikutoe hofu, lengo letu ni kuhakikisha kwamba maji yawe yanapatikana kwa wingi kwa kupitia mtandao wa zamani ambapo tunajua pia mtandao wa zamani una changamoto zake, lakini tutaendelea kujenga ule mtandao mpya, baadaye mpya utakapokamilika, mtandao wa zamani tunauondoa ili wananchi muda wote waweze kupata huduma ya maji safi na salama, ahsante.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 4
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Lusanga kina changamoto kubwa sana ya maji hasa Kitongoji cha Lusanga A, Kilingeni na Mkuyuni. Tunamshuruku Mheshimiwa Rais, tumepata mradi wa maji wa shilingi milioni 400, lakini mkandarasi toka amekabidhiwa site, ni miezi miwili hajarudi tena. Nini kauli ya Serikali juu ya huyu mkandarasi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jonas, Mbunge wa Mvomero na hakika sisi Wizara ya Maji tunaendelea kumshukuru kwa kutupatia ushirikiano mkubwa sana, pale ambapo kunapotokea changamoto ndani ya jimbo lake, amekuwa akituwasilishia kwa haraka sana na Wizara ya Maji imekuwa ikichukuwa hatua. Pia tunamshukuru kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya kwa kuwasemea wananchi wake wa Mvomero.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa tumeshapata mkandarasi baada ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia kutoa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kupeleka katika kijiji kile, na kweli mkandarasi ameshapatikana, lakini kulikuwa na changamoto hapa, lakini zimeshakamilika, zimeshafanyiwa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatumia fursa hii kwa niaba ya Waziri wa Maji kumwelekeza RM - Mkoa wa Morogoro ahakikishe mkandarasi huyu anafika site na kuanza kufanya kazi mara moja, ahsante sana.
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 5
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Ninaishukuru Serikali kwa kutupatia Mradi wa Maji wa Miji 28 wa shilingi bilioni 41. Je, Serikali haioni umuhimu sasa, kwa kuwa tunakwenda kuvunja Bunge la kuwatuma ama kuwaelekeza watendaji wakuu wa Wizara kama vile Katibu Mkuu kumtembelea mkandarasi yule ili kuhakikisha anamaliza mradi kwa wakati kwa maana ya kum-push?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Asenga kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajili ya wananchi wake wa Ifakara. Pia, tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, kama Wizara, watendaji wetu wataenda kutembelea na kuona namna gani mkandarasi anaendana na makubaliano yaliyopo kwenye mkataba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kuna mkataba lazima uheshimiwe. Wakati wa kuhitimisha mkataba ni lazima sisi kama Serikali tujue kabisa kwamba haendi nje ya mkataba ambao tunakubaliana. Kwa hiyo, nimtoe hofu kuwa watendaji wetu wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu, wataenda kuhakikisha kwamba mkandarasi huyo anaharakisha aweze kukamilisha kwa wakati. Ahsante sana.
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 6
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna chanzo cha maji ambacho kipo maeneo ya Magamba na wataalamu wakiongozana na Mkurugenzi wa RUWASA walienda kuona chanzo kile; na chanzo kile mradi wake ukitekelezeka utahudumia zaidi ya kata 15. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanza kujenga mradi huo? (Makofi
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kuna hiki chanzo, na kati ya vitu ambavyo ni vya muhimu sana kupata huduma ya maji safi na salama ni chanzo cha uhakika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kujiridhisha kwamba chanzo hiki kitaweza kuhudumia maeneo ambayo tumeyatarajia au tumeyaweka kwenye scope yetu ya kazi, basi hatua za kufanya upembuzi yakinifu huanza, na baada ya hapo tutafanya detail design na baada ya hapo tutajua gharama ya mradi na baada ya hapo tutafanya kazi ya kuhakikisha kwamba mradi huu unatekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Name
Lucy Thomas Mayenga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: - Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Supplementary Question 7
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenye Mikoa ya Tabora na maeneo mbalimbali ni mradi ambao ni wa kupongezwa sana, Serikali imefanya kazi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inaonaje iweze kuhakikisha wakati maji haya yanapotoka kule Ziwa Victoria Mwanza, kabla ya kwenda kwenye maeneo mengine; Tabora ni kwa ndugu zetu tunawapenda, lakini walau yaweze kupita na kufika kwenye maeneo ya karibu hasa Mkoa wa Shinyanga kwenye Jimbo la Kishapu kwa sababu kumekuwa kuna miradi ya maji, lakini ni kama ya kudokoadokoa? Wananchi wanalalamika sana kuhusu ukosefu wa maji katika Wilaya ya Kishapu na hasa Jimbo la Kishapu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa ninaiomba Serikali ije na mradi mkubwa ambao utagusa maeneo mengi katika wilaya hii ambayo ni kame.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhudumia Watanzania wote ambao wanatoka kwenye vyanzo vya maji na maeneo ambayo yamepakana na Ziwa victoria ikiwemo Shinyanga, Simiyu, Bariadi, Itilima pamoja na Busega.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais maelekezo yake yapo wazi kabisa. Kwa upande wa maji kwa bomba ambalo linapeleka Kahama pamoja na Tabora, tayari; Shinyanga hivi tunavyoongea tayari wanatumia maji ya kutoka Ziwa Victoria; vilevile katika Wilaya ya Kishapum tayari wanatumia maji ya kutoka Ziwa Victoria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichobaki kwa upande wa Kishapu kuna vijiji 11 ambavyo bado havijafikiwa na huduma hii ya maji ya kutoka Ziwa Victoria wanatumia visima. Kwa hiyo, mkakati wa Serikali ni kufanya extension kutoka bomba kuu la kutoka Ziwa Victoria kuhakikisha kwamba tunawasambazia wananchi waliopo katika Wilaya ya Kishapu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu dada yangu Mheshimiwa Lucy Mayenga, pia ninampongeza kwa kuendelea kuwasemea wananchi na wakina mama wa Kishapu. Pia, nimtoe hofu kuwa Serikali imelitazama kwa umakini sana na tayari kuna mradi ambao unaenda kuanza hivi karibuni kuhakikisha kwamba tunafanya extension kwa ajili ya vijiji hivyo 11 vya Jimbo la Kishapu. Ahsante sana.