Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi | 686 | 2025-06-25 |
Name
Oliver Daniel Semuguruka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE K.n.y. MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: -
Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwa ajili ya Kata za Gwanseli, Magata, Muleba, Bureza, Kikuku na Kagoma – Muleba utaanza?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye Kata Sita za Muleba, Magata/Kurutanga, Gwanseli, Bureza, Kikuku na Kagoma Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inaendelea na utafutaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo unaokadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 42. Aidha, katika mpango wa muda mfupi wa kuboresha huduma ya majisafi na salama katika kata hizo, Serikali imekamilisha utekelezaji wa miradi ya maji minne ya Ilemela, Magata/Kurutanga, Butembo na Kagoma inayohudumia wananchi 22,279 waishio kwenye Vijiji nane vya Ilemela, Gwanseli, Bureza, Butembo, Makarwa, Kikuku, Kagoma na sehemu ya Kijiji cha Nsisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hatua nyingine, Serikali imekamilisha mradi wa upanuzi wa skimu za maji ya Kurutanga na Butembo kwenda Kijiji cha Magata na Kitongoji cha Omdangara, Muleba Mjini ambapo huduma ya maji inawafikia wananchi wapatao 11,340, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved