Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo barabara ambayo inaunganisha mikoa mitatu, kwa maana ya Singida, Dodoma na Manyara. Barabara hiyo inatoka Manyoni inaingia Mpendo -Sanzawa – Kwa Mtoro – Lahoda hadi Hanang. Mpaka leo hii, pamoja na kuwa ni barabara inayounganisha mikoa mitatu, bado inahudumiwa na TARURA. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kuwa barabara hiyo inapandishwa hadhi na ijengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Monni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu uliopo, ili barabara iweze kupandishwa hadhi, Wakala wa Barabara ama Wizara ya Ujenzi huwa inapokea maombi kutoka kwenye mikoa husika, na hasa baada ya kuwa imejadiliwa kwenye vikao vya Road Board na RCC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimshawishi Mheshimiwa Mbunge kwamba wenzetu wa Mkoa wa Singida, Mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Manyoni, kwa maana inaunganisha mikoa hiyo, basi waweze kuleta hayo maombi Wizara ya Ujenzi, nasi tutaifanyia tathmini na ikikidhi vigezo itapandishwa hadhi ili iweze kuhudumia na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya interchange kutokea Zamahelo hadi Donsee ili kusudi iweze kuja kuungana na ile barabara ambayo ni ya Chemba hadi Singida?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hii barabara sina uhakika kama itakuwa ni interchange, lakini ukitoka Zamahelo kwenda Donsee ndiyo barabara ambayo inakutana na ile barabara ndefu ya kutoka Kibirashi kwenda Kwa Mtoro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokifanya kwenye hii barabara ni kuanza kuifanyia usanifu ili wananchi watakaokuwa wanatoka Chemba kama wanakwenda Singida wasilazimike kwenda huko. Kwa hiyo, wana uwezo wa kutokea hapa Zamahelo kwenda Donsee, halafu baada ya kukamilisha usanifu itakuwa ni kuijenga kwa kiwango cha lami.

Name

Kunti Yusuph Majala

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Barabara ya Kibirashi – Kwa Mtoro mpaka Singida ilikuwa inaambatana pamoja na ulipaji wa fidia kwa wananchi waliokuwa wanaathirika na barabara hiyo. Ametuambia hapa kwamba TPA pamoja na TANROADS wako kwenye michakato. Je, Serikali inawaambia nini Watanzania ambao wamepitiwa na barabara hiyo kwa ajili ya ulipaji wa fidia ili mchakato utakapokamilika barabara hiyo isilete tena kikwazo kwa ajili ya fidia kwa wananchi wetu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, pale ambapo fidia inahitajika, Serikali haianzi ujenzi mpaka iwe imekamilisha usanifu. Tunachofanya sasa hivi ni kwamba watu watafanyia tathmini, na ukishafanyiwa tathmini watalipwa ndipo ujenzi utakapoanza; lakini wakati tunafanya hizi shughuli, hazizuii kuendelea na taratibu nyingine za TPA na TANROADS kufanya kuingia kwenye mazungumzo ili tuanze kuijenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwahakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi watakaoathirika na barabara hiyo kwamba watalipwa mafao yao kwa maana ya fidia kabla hatujaanza ujenzi wa hiyo barabara.