Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 684 | 2025-06-25 |
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mrijo – Chemba – Kwamtoro hadi Singida kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kiteto – Mrijo – Chemba hadi Singida yenye urefu wa kilometa 461 kwa awamu ambapo kwa sehemu ya kwanza Handeni – Mafuleta (kilometa 20) ujenzi umefikia asilimia 46.06.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, sehemu ya pili ya Mafuleta – Kileguru (Km 30) na Kibaya – Kisima (kilometa 50) makandarasi wapo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wako kwenye majadiliano ya awali ya kuijenga kwa utaratibu wa PPP, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved