Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ilongero

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igauri Km 11.5 – Ilongero hadi Haydom Km 80 kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa fursa ili niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, ninashukuru kwa maelezo hayo yanayotia moyo ya kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ningependa kujua; kwanza, mchakato huu kidogo umekwishakuwa wa muda mrefu, Je, Mheshimiwa Waziri anatoa kauli gani kwa TANROADS na kwa Meneja wa TANROADS wa Mkoa, kuhakikisha kwamba huu mchakato unaharakishwa uende haraka ili ujenzi uweze kuanza haraka iwezekanavyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, katika mwaka wa fedha 2022/2023 tukiwa hapa Bungeni niliwahi kuuliza kuhusu ujenzi wa kiwango cha lami wa kipande cha barabara ya Ilongero - Ikhanoda hadi Ngamu kwa kiwango cha lami, ambacho nacho kinatuunganisha sisi na Manyara, nataka kujua, je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha barabara hiyo sasa na yenyewe ujenzi unaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, suala la manunuzi linaweza likachukua muda mfupi ama muda mrefu kulingana na wale walioomba kazi. Wakati fulani wanaweza wakaomba wakandarasi ambao hawana sifa, kwa hiyo, unaweza ukatangaza upya. Ama wakaomba, lakini kukawa na bei kubwa, ambayo kwa utaratibu uliopo haiwezi ikakubalika. Kwa hiyo, lazima itachukua muda kukaa nao ili kuweza kupunguza bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kazi iliyopo sasa hivi, tuko kwenye majadiliano na wakandarasi ambao wameomba. Mimi nitoe maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Singida na Makao Makuu TANROADS kuhakikisha kwamba suala hili linafanyiwa uharaka ili ujenzi uweze kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, la Ilongero – Ngamu barabara ambayo ina takribani kilometa kama 27, kitu tutakachokifanya ni kuweka kwenye mpango ili kwanza iweze kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mwaka wa fedha unaokuja.

Name

Luhaga Joelson Mpina

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisesa

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igauri Km 11.5 – Ilongero hadi Haydom Km 80 kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imekamilisha kufanya upembuzi yakinifu wa barabara ya kutoka Bariadi – Itilima – Kisesa – Mwandoya – Mwanhuzi – Bukundi – Mkalama – Iguguno hadi Singida, je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza sasa? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipande alichataka cha kuanzia Iguguno hadi Itilima viko vipande ambavyo viko tayari kwenye hatua za kuanza ujenzi, kwa maana ya manunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa kuwa ndiyo kwanza tumekamilisha upembuzi yakinifu, na sasa Serikali katika mwaka wa fedha unaokuja itabidi ipange, tutakuwa sasa tunaipangia kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Isingekuwa rahisi kuipanga wakati usanifu bado haujakamilika.

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igauri Km 11.5 – Ilongero hadi Haydom Km 80 kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwanza, kabisa ninaishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara ya kuanzia Dumila mpaka Kilosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ninatambua kuwa kuna ujenzi unaoendelea kwenye kipande cha barabara pale Ulaya kwa kiwango cha lami. Je, ni lini kipande kilichobaki kuanzia Kilosa mpaka Mikumi kitajengwa kwa kiwango cha lami, kwani wakati wa mvua hii barabara ni mbovu sana?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kwa kuwa mvua imekatika, nimwelekeze Meneja wa Mkoa ahakikishe mkandarasi aliyepangiwa kazi aende akarekebishe maeneo yote yaliyokuwa korofi ama yaliyoharibika ili magari yaweze kupita katika hali ambayo ni nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuikamilisha hii barabara, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama kuna barabara ambayo sasa ni kipaumbele cha Serikali ni Kilosa - Mikumi kwa sababu ndiyo inayounganisha karibu ukanda huu wa Njombe kama tutakamilisha kutoka Ruvuma ili watu wasiende Morogoro wakishafika Mikumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali inatafuta chanzo madhubuti ama chanzo kizuri, ikiwa ni pamoja na kuangalia fedha za wahisani ili tuweze kuijenga hiyo barabara ya kuunganisha Mikumi – Kilosa hadi hapa Dumila kwa kiwango cha lami.

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igauri Km 11.5 – Ilongero hadi Haydom Km 80 kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 4

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa nafasi. Barabara ya Kiranjeranje - Nanjirinji mpaka Ruangwa imekamilika kufanyiwa upembuzi na usanifu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami angalau kutoka Kiranjeranje mpaka Makangaga?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tumekamilisha kuifanyia usanifu barabara hiyo, lakini Mheshimiwa Mbunge atakubaliana nao kwamba barabara hiyo ina madaraja kama matatu ambayo ni korofi, ambayo mvua ikinyesha hayapitiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichofanyika katika Awamu hii ya Sita ni kwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha kujenga Daraja la Mbwemkuru. Ukishamaliza hili Daraja la Nakiu kwenda Kiranjeranje imekuwa ni changamoto kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwanza tunahakikisha kwanza tunayajenga hayo madaraja yote matatu wakati tunatafuta fedha sasa za kujenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami.