Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi | 683 | 2025-06-25 |
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ilongero
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igauri Km 11.5 – Ilongero hadi Haydom Km 80 kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Igauri – Ilongero hadi Haydom ni barabara ya mkoa inayojulikana kwa jina la Singida Urban – Ilongero – Haydom (kilometa 93.8). Ujenzi wa Barabara hii kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa jumla ya kilometa 12.5 kutoka Singida eneo la Njuki hadi Igauri zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ipo katika hatua za mwisho za manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa sehemu ya Igauri – Ilongero (kilometa 18.5). Kwa sehemu iliyobaki ya kutoka Ilongero hadi Haydom (kilometa 69.8), Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved