Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati au kuliongeza Gereza la Keko?
Supplementary Question 1
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nishukuru sana kwa jinsi ambavyo fedha hizi zimeweza kushushwa. Sina swali la nyongeza, lakini napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Serikali yake ya Chama cha Mapinduzi kwa jinsi ambavyo hakika tumeweza kuomba na fedha hizi na zimeshuka. Muhimu ni kwamba, tunaomba sasa Jeshi la Magereza lifanye kazi kwa udhibiti, ili gereza lile lipate kuwa na usafi na usalama.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Dorothy Kilave, Mbunge wa Temeke, kwa ufuatiliaji wake. Pia, namshukuru sana kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukarabati wa magereza mbalimbali hapa nchini. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati au kuliongeza Gereza la Keko?
Supplementary Question 2
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Gereza la Wilaya ya Mbulu limejengwa toka enzi za koloni. Kwa Bahati nzuri na Serikali imekuwa na mipango mizuri ya kukarabati magereza haya kongwe nchini. Mpango ukoje kwa magereza yote nchini, likiwemo Gereza la Wilaya ya Mbulu, katika ukarabati na ujenzi wa makazi ya Askari na jengo la magereza? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kila mwaka wa fedha tunatenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa magereza mbalimbali. Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 tulitenga shilingi bilioni 6.272, kwa ajili ya ukarabati wa magereza haya. Tumeanza na Gereza la Keko, Ukonga, Segerea pamoja na Gereza la Lilungu liliopo Mkoa wa Mtwara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge pia, kama nilivyosema, tunatenga fedha kila mwaka. La Mbulu pia, tutalichukua tuliingize kwenye mpango, tayari kwa ajili ya kutengewa fedha ya ukarabati. Ahsante sana.
Name
Maryam Omar Said
Sex
Female
Party
CUF
Constituent
Pandani
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati au kuliongeza Gereza la Keko?
Supplementary Question 3
MHE. MARYAM OMAR SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hali isiyoridhisha ya makazi ya Askari wa Finya, Basara pamoja na Wetelaini, ni lini Serikali ifanya ukarabati mkubwa wa makazi hayo?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka na kufanya ukarabati wa makazi ya Askari wetu. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, pia maeneo aliyoyataja ya Finya pamoja na Wete wataalamu wetu wataenda kufanya tathmini, ili kuona kiasi kinachotakiwa na kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati. Askari wetu wakae katika mazingira salama kwa ajili ya kulinda raia na mali zao. Ahsante sana.
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya ukarabati au kuliongeza Gereza la Keko?
Supplementary Question 4
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, uwepo wa magereza katika maeneo mbalimbali umesaidia sana kuongeza nguvukazi, hasa katika masuala ya usafi na mambo mengine, maeneo ya miji. Je, ni lini Gereza la Wilaya ya Nyasa, ambalo tayari Wizara imeshalipa fidia, litaanza kujengwa ili pia, Nyasa inufaike na uwepo wa magereza?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya kwa ufuatiliaji wake wa Gereza la Nyasa. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tayari kama ambavyo Serikali imelipa fidia, ndiyo hiyo hatua ya kwanza. Kulipia fidia ni kuwaondoa wananchi katika eneo hilo na sasa hatua inayofuata ni kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Gereza la Nyasa. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved