Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 53 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 681 2025-06-25

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: -

Je, lini Serikali itafanya ukarabati au kuliongeza Gereza la Keko?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza la Mahabusu Keko ni miongoni mwa Magereza yaliyojengwa katika kipindi cha ukoloni, mwaka 1957. Serikali kupitia Jeshi la Magereza imepokea fedha kiasi cha shilingi 988,125,000.00 kilichotengwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, kwa ajili ya ukarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Jeshi la Magereza linaendelea na hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya kuanza kazi ya ukarabati wa gereza hilo, ahsante.