Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini pia niseme kwamba Mji wa Arusha ulikuwa na viwanda vingi sana. Kwa kifupi, kufa kwa viwanda hivi wananchi wamepoteza ajira na mapato. Kuna viwanda vingine ambavyo vilikufa tu hivi katika mazingira ambayo hatukujua. Kwa mfano, Kiwanda cha Kilitex, Kiwanda cha Kiko, Kiwanda cha Kuchakata Pareto, na vingine vilikufa. Je, Serikali inasemaje kuhusu kufufua hivyo viwanda sasa hivi? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, ukiangalia nchi yetu rekodi tulikuwa na viwanda vingi sana vya kihistoria. Baba wa Taifa alitengeneza viwanda vya kimkakati, lakini ilikuwa nia njema ya Serikali ya kufanya ubinafsishaji wa viwanda hivyo, lakini kwa bahati mbaya sana maeneo mengi viwanda hivyo hatukufikia malengo tuliyofikia. Ndiyo maana Serikali sasa hivi tunafanya analysis katika mikoa mbalimbali, na tayari timu yetu imeanza katika mikoa mbalimbali ukianzia Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Tanga, lakini inaenda katika mikoa yote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kubwa ni kuhakikisha tunakamilisha ule mpango mkakati wa viwanda 9,045 tunavyotarajia kutengeneza ndani ya miaka mitano hii, ndani yake ikiwepo kufufua viwanda vyote ambavyo vimetelekezwa na wawekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba niwahakikishie wananchi wa Kilimanjaro, wananchi wa Arusha na kote Tanzania kwamba, Serikali imeamua kuliweka jambo hili kimkakati, na tushukuru sana Ofisi ya Msajili wa Hazina inatupa ushirikiano wa kutosha kuona jinsi ya kufikia malengo mapana kuhakikisha viwanda hivi vyote vinafufuliwa na hasa wale waliokuwa na nia ovu ya kuchukua viwanda na kuvifanya Collateral katika upatikanaji wa fedha. Kwa hakika tumejipanga, hatutakubali katika eneo hilo. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 2
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Wilaya ya Hanang, Kata ya Mogitu ina malighafi ya kutosha kabisa kwa ajili ya utengenezaji wa cement. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuleta wawekezaji pamoja na kuwezesha wananchi ili kuanzishwa kiwanda cha cement, kwa sababu malighafi hiyo ipo ya kutosha kwa zaidi ya miaka 50? Je, Serikali ina mpango gani kuja kuwekeza sasa ili kuona cement hiyo na malighafi hiyo inaleta tija kwa wananchi wa Hanang, na pia kwa Taifa letu la Tanzania? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kushukuru na nimpongeze dada yangu Mheshimiwa Asia kwa sababu amekuwa Mbunge machachari sana na wananchi wa Mkoa wa Manyara wanajivunia yeye, kijana machachari na shupavu sana. Hongera sana dada yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la malighafi inayopatikana Mkoa wa Manyara, especially eneo la Hanang. Ni kweli, nchi yetu hivi sasa katika mpango wa viwanda, tumejielekeza kwanza kuangalia malighafi tulizonazo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri Mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Manyara una fursa kubwa sana kwa ajili ya kuzalisha madini ya Iron Ore, ambayo yanatumika katika uzalishaji wa cement. Hivi karibuni, bahati nzuri juzi tu, nilikuwa na mwekezaji ambaye anakuja kuangalia eneo la kimkakati kati ya Manyara na Dodoma kutengeneza kiwanda kikubwa cha cement kwa lengo la kutumia malighafi iliyopo hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutachagiza eneo hili, hasa kuwahamasisha wawekezaji fursa hiyo iweze kutumika vizuri kwa maslahi mapana ya uchumi wa mtu mmoja mmoja katika eneo la Hanang na Mkoa wa Manyara, Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imani yetu kubwa, kama nilivyosema hapa juzi kwamba nchi yetu sasa hivi production ya cement imeenda vizuri, sasa tunazalisha tani milioni 10 na demand yetu ni tani milioni saba. Tunataka tu-expand kabisa eneo hilo la sekta, ili tuweze ku-export katika nchi nyingine tupate fedha za kigeni. Hiyo ndiyo target yetu kama nchi.
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 3
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Je, Serikali ina mpango gani wa kusaidia kufufua kiwanda cha kimkakati cha kuzalisha dawa za kilimo cha Twiga Chemical kilichopo Mjini Moshi?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze sana Profesa, watu wa Kilimanjaro wanajivunia yeye, kwani amekuwa mbobezi mahiri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda hiki, kama target yetu, tumeanza kufanya mapping katika Mkoa wa Kilimanjaro kubainisha viwanda vyote. Kwa mfano, hapa utasikia Kiwanda cha Kibo, Kilimanjaro ilikuwa na utajiri mkubwa sana wa viwanda. Hii ndiyo miongoni mwa changamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, katika eneo ambalo tunataka tulifanyie kazi na hasa ukiangalia katika kipindi cha sasa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kufanya investment kubwa sana katika upande wa sekta ya Kilimo. Maana yake ni nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende tufikie muda tusi-import, baadhi ya dawa tuzalishe hapa nchini. Kwa hiyo, hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo naomba nikuhakikishie katika mpango wetu mkakati ule wa viwanda 9,045 ikiwa ni pamoja na kufufua vile viwanda ambavyo mwanzo vilikuwa vinafanya kazi, lakini sasa hivi havifanyi kazi, na eneo hilo la Twiga Chemical Limited tutalifanyia kazi kwa nguvu zote. Ahsante sana.
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 4
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Tunajua lengo la Serikali kutenga hivyo viwanda zaidi ya 900, naamini ni pamoja na kuendeleza yale maeneo ambayo wananchi walitenga ya EPZA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Jafo anajua, nilisema, kwetu Jimbo la Bunda Mjini, Kata ya Guta, eneo la Tailo, ni zaidi ya miaka 17 wananchi wamelipwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ambavyo vitachangia ajira katika Jimbo la Bunda Mjini, Halmashauri pamoja na Wilaya nzima ya Bunda na Mkoa wa Mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua, ni lini sasa watajenga viwanda kutokana na malighafi zinazopatikana Mkoa wa Mara na Jimbo la Bunda Mjini? Kuna wafugaji, kuna wavuvi, tunalima pamba na mambo mengine. Ni lini sasa watatujengea viwanda, ili akinamama na vijana waweze kupata ajira? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze UVCCM mwenzangu, dada yangu, Mheshimiwa Ester Bulaya alikuwa Lumumba pale, amefanya kazi kubwa sana katika Redio Uhuru na maeneo mengine. Ni miongoni mwa vijana waliokuwa shupavu sana wakati ule, comrade Masauni akiwa Mwenyekiti. Namshukuru sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hilo kwanza target yetu ni kweli, tuna maeneo mengi tuliyatenga kwa ajili ya kuhakikisha tunawekeza viwanda, siyo Mara peke yake, hata katika Mkoa wa Tanga na maeneo mengine. Kwa hiyo, nakuhakikishia kwamba, mpango huu Serikali tunaondokanao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tutabainisha yale maeneo ambayo Serikali tuliyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, na inawezekana tulilipa fidia, lakini sehemu nyingine fidia haijalipwa. Hivyo, mpango mkakati ni wa kujenga industrial parks na clusters mbalimbali, tunaenda kufanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwaambie wananchi wa Mkoa wa Mara, kama Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyojipanga kimkakati, tutashughulikia maeneo yote kwa kipaumbele kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanaleta tija kwa vijana wetu ambao ni wengi. Sasa hivi ni graduates, wanamaliza vyuo vikuu waweze kupata ajira kupitia Sekta ya Viwanda. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 5
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa issue ya fidia, maeneo ya Yombo katika Wilaya ya Bagamoyo, wamekaa kwa muda mrefu sana pasipokulipwa fidia. Ni lini watu hawa watalipwa fidia ikiwa maeneo haya yamechukuliwa na Serikali kwa muda mrefu? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Mheshimiwa Mchungahela, kwa kuuliza eneo la Bagamoyo. Kubwa zaidi naomba nikuhakikishie kwamba, ni mpango wa Serikali kuhakikisha eneo la Bagamoyo linaenda kuwa nyeti kwa Taifa letu katika mpango mkakati wa viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni katika mpango huo kuna maeneo mengine yamelipwa fidia na maeneo mengine hayajalipwa. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa hivi amesikia Waziri wa Mipango alikuja na mpango mkakati mkubwa sana wa suala zima la ujenzi wa viwanda na hasa upande wa Bagamoyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwahakikishie wale ambao hawajalipwa fidia, provided kwamba wapo katika taratibu zile ambazo zimeainishwa na Serikali, kila mtu atapata haki yake ile inayostahili. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 6
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumwuliza Mheshimiwa Waziri, Wilaya ya Ilemela Eneo la Nyamanoro, ilitenga eneo kwa ajili ya industrial park na andiko tayari lilishakuja Wizarani, na mwaka juzi liliingia kwenye utaratibu wa mchakato, lakini mpaka sasa ni kimya. Napenda kujua ni lini industrial park hiyo itajengwa; kwa sababu, miundombinu yote ya umeme na barabara ipo vizuri? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze mtani wangu, bibi yangu, Mheshimiwa Angeline Mabula, kutoka Wilaya ya Ilemela. Ni kweli, nashukuru eneo hilo la Ilemela, mimi na yeye kipindi kile tulienda pamoja, wakati ile timu ya Mawaziri, hasa upande wa karibuni na uwanja wa ndege.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwahakikishie kwamba, katika mipango ambayo tumeweka ya kuainisha maeneo ya ujenzi wa industrial park na tunafahamu kwamba, Kanda ya Ziwa tunatumia bidhaa nyingi kutoka nchi jirani, tuna kila sababu ku-establish hub kubwa ya viwanda eneo hilo. Lengo ni kupunguza importation ya bidhaa kutoka nchi za jirani na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia dada yangu, bibi yangu, Mheshimiwa Angeline Mabula, tutalifanyia kazi eneo hili na hasa, mahususi, eneo la Mkoa wa Mwanza katika Wilaya ya Ilemela. (Makofi)
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Supplementary Question 7
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kuwa, Mheshimiwa Waziri amesema kuna mwekezaji anataka kuja Manyara na sisi Kiteto tupo tayari kumpokea, lini atamleta Kiteto? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Wakili Msomi, kaka yangu, Mheshimiwa Olelekaita na ninamombea sana watu wa Kiteto wamrudishe, amefanya kazi kubwa sana, amelielimisha Bunge hili sana. Elimu yake ya usomi wa sheria imetusaidia sana kama Bunge la Tanzania, na watu wa Manyara wasikie kwamba tuna Mbunge makini kutoka katika Wilaya ya Kiteto. Hongera sana ndugu yangu Mheshimiwa Olelekaita. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo hili maana yake ni watu wanafanya needs assessment katika maeneo haya. Tutahakikisha maeneo yote wanayapitia na ninaamini katika kanda hii tutapata kiwanda kimoja kikubwa, provided kokote kitakapojengwa kitasaidia wananchi wa kanda hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, imani yetu kama Serikali ni tutachagiza kuwapata watu hawa wafike, wabainishe maeneo, waweze kuwekeza. Kwa hiyo, naomba niwawahakikishie watu wa Manyara na Dodoma, tunahangaikia ujenzi wa kiwanda kikubwa cha cement hapa, lengo kubwa ni kutumia Iron Ore iliyopo, kuzalisha malighafi ya cement, hasa kuzalisha cement for export katika maeneo mengine. (Makofi)