Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 680 | 2025-06-25 |
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua Viwanda vya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) na General Tyre?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango wa kufufua viwanda vyote nchini ambavyo havifanyi kazi kwa sasa ili kujiepusha na gharama kubwa za uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, upotevu wa ajira, na upotevu wa fedha za kigeni za kuongeza mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries, kupitia Serikali, Msajili wa Hazina anashirikiana na mwekezaji kukifufua kiwanda hicho, na kwa sasa kipo hatua za mwisho za kuanza ukarabati wa kiwanda pamoja na mitambo; na baada ya ukarabati huo kukamilika, uzalishaji utaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kiwanda cha General Tyre, Serikali kupitia Shirika la Mandeleo la NDC inatafuta mwekezaji wa kimkakati ili kuanza uzalishaji wa matairi ya magari hapa nchini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved