Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI auliza: - Je, nini faida na hasara ya Tanzania kutokana na msimamo wa Nchi za BRICS ambazo zimejipanga kujiondoa kwenye Mfumo wa Dollarisation?
Supplementary Question 1
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaomba niishukuru Serikali kwa majibu mazuri na ambayo kwa kweli nilitegemea ndivyo yatakavyokuja. Naomba niishauri Serikali baada ya kuuliza swali la msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, BRICS ni Economic Alliance na duniani sasa tuna kitu tunaita Economic Intelligence. Kwa hiyo, ningeiomba na kuishauri sana Serikali, kwa sababu hii vita ni vita kubwa na real, ina uwezo wa kutengeneza uchumi na kuuangusha siku moja tu, ninadhani ushahidi wanao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali na hasa wale wataalamu wetu wa mambo ya uchumi na fedha, hebu waende wakakae wafanye tathmini kwa sababu kushiriki kwetu kama washirika tu kwenda kuangalia mikutano, lazima kuwe na tija ndani yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeomba waangalie kwa sababu kwa kweli hii ni vita ni ya kiuchumi, na sisi kama Tanzania tusije tukaachwa nyuma tujikaona kama ni wasindikizaji. Ninakushukuru sana. (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba nimpongeze na kumshukuru sana Mheshimiwa Zahor kwa kuwa mara nyingi ushauri wake unakuwa ni wa kujenga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Zahor kwamba, ushauri wake tumeuchukua na Serikali itaufanyia kazi
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved