Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 53 | Finance | Wizara ya Fedha | 679 | 2025-06-25 |
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI auliza: -
Je, nini faida na hasara ya Tanzania kutokana na msimamo wa Nchi za BRICS ambazo zimejipanga kujiondoa kwenye Mfumo wa Dollarisation?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa na ushirikiano wa karibu wa muda mrefu na nchi za BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) katika nyanja mbalimbali ikijumuisha masuala ya kiuchumi, biashara, na diplomasia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahusiano hayo yanadumishwa kwa kuendelea kuwepo kwa Balozi za nchi hizo hapa nchini na Tanzania kuwa na Balozi katika nchi hizo. Mahusiano hayo yanaendelea kuleta mafanikio chanya kwa Serikali ya Tanzania kwa kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika nchi hizo ambazo pia zinaimarisha mahusiano ya uwili baina yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Tanzania siyo mwanachama wa BRICS ila inashiriki katika mikutano ya BRICS kama observer. Hivyo, mafanikio au changamoto zozote katika umoja huo zinazoweza kutokea katika sekta ya kiuchumi na fedha hususan ya kujiondoa kwenye Dollarisation, Tanzania hatutakuwa na athari za moja kwa moja kwa kuwa sio wanachama wa BRICS. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved