Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kudhibiti vumbi la makaa ya mawe yanayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara?

Supplementary Question 1

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Ni kwa kiwango gani Serikali imetoa elimu na vifaa stahiki kwa wale vibarua na wafanyakazi ambao wanashughulika pale bandarini ili kuwakinga na athari zitokanazo na vumbi hilo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa Bandari ile ya Mtwara bado inatumika na siyo kule ambako kunajengwa bandari kwa sababu bado haijakamilika, ni kwa namna gani wafanyakazi wanaofanya kazi pale bandarini wanakingwa ili wasiathirike kutokana na hiyo vumbi ya makaa ya mawe? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kwanza kumpongeza na kumshukuru sana kwa kazi nzuri anayoifanya, lakini kubwa zaidi kwa kutaka kuona namna ambavyo Serikali inatatua changamoto za kimazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo hatua mbalimbali ambazo Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na NEMC, kwa kushirikiana na wenzetu wa TAMISEMI, OSHA, bandari na taasisi nyingine ambazo kwa namna moja ama nyingine zinahusika, tumechukua katika kutoa elimu na kuwaelimisha wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni kuhakikisha kwamba tunawaelimisha wananchi hasa wafanyakazi wa maeneo hayo juu ya masuala mazima ya matumizi ya vifaakinga ambavyo vinaweza vikawasaidia kuepukana na athari kubwa ya vumbi linalosababishwa na mkaa ama makaa ya mawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi ni elimu ya usalama mahali pa kazi. Tumekuwa tukiwapa elimu mara kwa mara wenzetu wa bandari, hasa na wananchi ambao wanazunguka maeneo hayo. Pia, kubwa zaidi tumekuwa tukiwaelekeza, kuwasimamia na kuwasisitiza kuwa wote wanaomiliki magari yanayopakia mkaa wa mawe kuhakikisha kwamba wanafunika ili mavumbi yasitoke yakaenda kuathiri wananchi. Kikubwa tumekuwa tunatoa elimu ya uchimbaji na namna ambavyo tunaweza tukasimamia sheria za mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ni kweli kumekuwa kuna changamoto hasa kwenye athari ya bandari. Moja ni kwamba, kama alivyosema na kama tulivyoeleza katika jibu la msingi, sasa hivi bandari imeshaanza kujengwa ingawa haijakamilika, lakini itakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari hii itakapokamilika maana yake ni kwamba magari yote ambayo yatabeba mkaa wa mawe na bidhaa nyingine chafuzi za mazingira hayatapita eneo la makazi na yatapita mbali ili wananchi wasiweze kuathirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi na tunaendelea kutumia mitambo maalumu ambapo mtambo huo hautafanya magari yaingie baharini au bandarini. Pia mtambo huo ndiyo utakaobeba mizigo kuingiza kwenye bandari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. (Makofi)

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kudhibiti vumbi la makaa ya mawe yanayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara?

Supplementary Question 2

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Changamoto iliyokuweko Mtwara ndiyo iliyokuweko Zanzibar, ya vumbi la saruji na bidhaa nyingine ambazo zinatumia bahari. Je, Serikali mna mpango gani wa kushughulikia changamoto hiyo? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba pia nijibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Abdul Maalim, Mbunge na mtumishi wa wananchi wa Jimbo la Amani. Naye nimpongeze kwa kazi kubwa anayoifanya, hasa ya kutaka kujua namna ambavyo Serikali tumejipanga katika kutatua changamoto za kimazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zipo hatua mbalimbali ambazo zimechukuliwa. Moja ni kubwa la mwanzo ni la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, kwa sababu ni kweli, kama saruji na kule inashushwa, kama ni gypsum kule pia inashushwa, na kama baadhi ya bidhaa nyingine ambazo zinaweza kuwa ni chafuzi nazo zinashushwa kupitia bandari tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumekuwa tukitoa elimu, hasa elimu ya mazingira ya kazi kwa wananchi na hasa wafanyakazi wa hapo. Kikubwa Mheshimiwa Dkt. Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefanya ukarabati wa bandari nyingi sana ambapo bandari nyingi sasa zimeanza kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo Bandari ya Mpigaduri inajengwa, lakini ipo Bandari ya Mwangapwani. Bandari hizi zitapunguza msongamano wa mizigo kushushwa sehemu moja na badala yake ikawa kuna sehemu ya abiria na kuna sehemu ya mizigo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. (Makofi)