Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 53 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 678 2025-06-25

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kudhibiti vumbi la makaa ya mawe yanayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kudhibiti vumbi la makaa ya mawe yanayosafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua hizo ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa bandari nyingine nje ya Manispaa ya Mtwara Mikindani katika eneo la Kisiwa Mgao ambapo bandari hiyo itatumika kusafirisha bidhaa chafuzi kwa mazingira, kama vile simenti na makaa ya mawe. Hivyo, magari yote yanayobeba makaa ya mawe yatapita nje ya Manispaa kuelekea bandarini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua nyingine ni pamoja na kutumia mitambo miwili yenye uwezo wa kupakia tani 600 kwa saa ambayo ina mikanda maalum (Conveyor Belt) kwa ajili ya kupakia mzigo kwenye meli, kuweka nyavu za kuzuia vumbi, kuhakikisha magari yote yanayosafirisha makaa ya mawe yanafunikwa ili kuzuia vumbi lisisambae kwenye mazingira, na kunyunyuzia maji mara kawa mara katika eneo la hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.